TUZO ZA WATUMIAJI WA HUDUMA AFRIKA 2022 ZAZINDULIWA


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzanina (TANTRADE) Bi. Latifa Mohamed Khamisi akizungumza katika hafla fupi ya uzinduzi wa Tuzo za Chaguzi za Watumiaji Afrika (TCCA) kwa mwaka 2022 jijini Dar es Salaam.

Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Tuzo za Chaguzi za Watumiaji Afrika (TCCA), Diana Simon Laizer akizungumza katika hafla fupi ya uzinduzi wa tuzo hizo jijini Dar es Salaam. 

NA ABRAHAM NTAMBARA

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzanina (TANTRADE) Bi. Latifa Mohamed Khamisi amezindua Tuzo za Chaguzi za Watumiaji Afrika (TCCA) kwa mwaka 2022.

Akizungumza katika hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika leo Juni 7, 2022 jijini Dar es Salaam Bi. Latifa amempongeza Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Tuzo hizo Diana Simon Laizer kwa ubunifu wake unaolenga kuchochea ubora wa huduma.

Bi. Latifa amesema kwamba tuzo hizo ni kichocheo cha maendeleo ya biashara na huduma bora kwa watumiaji, hivyo ni jambo la kuungwa mkono.

“Tuzo hizi ni zakipekee na zinaongeza ushindani na viwango bora vya utoaji huduma kwa watumiaji. Niahidi kwamba Serikali itashirikiana na wewe katika kuhakikisha tukio hili linaendelea kuwa kubwa zaidi,” amesema Bi. Latifa. 

Kwa upande wake Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Tuzo za Chaguzi za Watumiaji, Diana Laizer amesema kuwa ni heshima kumpa watumiaji wa Tanzania na Afrika kwa ujumla nguvu ya kuchagua ni kampuni gani inayotoa huduma bora.

Ameishukuru Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuunga mkono mpango huo kupitia TANTRADE.

“Serikali inaunga mkono juhudi zetu kwa miaka mitatu na katika mwaka huu wa nne tunatarajia kiwango cha juu cha ushiriki kupiga kura kwa kampuni zinazotoa huduma zao bora,” amesma Laizer.Aidha ameongeza kwamba lengo la tunzo hii nikufikisha sauti ya walaji kuhakikisha wazalishaji wanatoa huduma bora zinazokidhi matakwa ya watumiaji.

Amebainisha kuwa tunzo hizo za kimataifa zitajumuisha vipengele 20 mojawapo ni pamoja na huduma za kifedha, Bima, huduma za hoteli, ujenzi sambamba na mitandao ya simu.

TCCA ni hafla ya kwanza nchini ambayo inajumuisha washiriki kutoka Bara zima la Afrika na zaidi kwa kupiga kura kwa kampuni ambazo watumiaji wanahisi zinatoa huduma bora.

Watumiaji wanweza kushiriki kwa kupiga kura kupitia jukwa la TCCA www.ccawardsafrica.co.tz.

Post a Comment

0 Comments