Na Mwandishi Wetu
JAMII imetakiwa kushirikiana na serikali katika kuwasaidia wanafunzi nchini wenye mahitaji ili waweze kujiendeleza kielimu.
Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Sondole Bulenga ambaye ni Katibu wa Sumani Foundation ambayo inajihusisha katika kutoa msaada kwenye Afya na elimu wakati wa mkutano wa kuwashukuru wafadhili wanayoisaidia taasisi hiyo.
Bulenga amesema Serikali peke yake haiwezi kufanya kila jambo hivyo ni wajibu wa jamii kutoa misaada kwa wanafunzi.
"Tuomba jamii ikiwezekana wakawasiliana na sisi wakaleta misaada,serikali ina mambo mengi na sisi kama sisi tuungane kuitengeneza jamii ya watoto wengine watakaosadia"Amesema.
Akizungumzia kuhusu Foundation hiyo,Bulenga,amesema kwa kipindi cha miaka miwili wameweza kuwasaidia wanafunzi nchi hasa katika nyaja ya afya na elimu.
"Wengi wamekuwa wakitusapoti na sisi tunanunua madawati,na tumeona mahitaji mengi wako watoto wanahitaji chakula,taulo za kike"Amesema.
Kwa Upande wake aliyekuwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Yongwe iliyopo Chanika Jijini Dar es salaam,John Sospiter,ameipongeza Foundation hiyo kwa misaada mbalimbali katika shule hiyo na kusema misaada hiyo imekuwa chachu kwao kufanya vizuri.
"Kwa kipindi kirefu wametusaidia mazingira ya shule na kuwa ya mfano upatikanaji madawati 250,kutuwekea umeme kwenye madarasa,upatikanaji wa Uji kwa wanafunzi"Amesema.
Hata hivyo,Mwalimu Sospita,amewataka watu wengine kuiga kwa mfano wa foundation kwa kutoa misaada kwa jamii,na kusema misaada hiyo inachangia kuinua elimu nchini.
Huku naye Joicy Jummanne ambaye ni mwanafunzi wa Darasa la saba katika shule hiyo,ameipongeza Foundation hiyo kwa msaada mkubwa ikiwemo wa Chakula na kuwaletea walimu.
0 Comments