ZAIDI YA WANANCHI 35 WAPATIWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KATA YA NANGA.



Mwakilishi wa vijana Taifa TWCC  na Mkurugenzi  wa  MUMAKI Products Mwalimu Maria Isdory akiwafundisha wananchi zaidi ya 35 wa kata ya Nanga wilayani Igunga walionitokeza katika mafunzo ya siku moja ya utengenezaji wa mafuta ya mgando na sabuni ya kufulia ya maji, vifaa na matilio yanavyotumika, kanuni, taratibu za uandaji wa utengenezaji wa bidhaa hizo.

Na Lubango Mleka, Igunga. 

WANANCHI zaidi ya 35 wa Kata ya Nanga Wilaya Igunga Mkoani Tabora wamepatiwa elimu ya mafunzo ya ujasiriliamali wa utengenezaji wa mafuta ya mgando ya kujipaka, sabuni ya maji ya kufulia na sabuni ya maji ya usafi wa chooni, ofisini na nyumbani.

Mafunzo haya yamefanyika ofisi ya mtendaji kata ya Nanga na kushirikisha makundi ya rika mbalimbali ya vijana wa kike na kiume, watu wazima na wazee na yakuwa na lengo la kuwakomboa wananchi kiuchumi, kuachana na utegemezi na kujiajili wenyewe kupitia kazi za mikono ambazo zitawainua kiuchumi kwa kujipatia kipato baada ya kujifunza.

"Nimeamua kufanya mafunzo haya bure kwa lengo la kuunga juhudi zinazofanywa na Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, viongozi wa TWCC, Mkuu wa wilaya ya Igunga Sauda Mtondoo na Mkurugenzi wetu mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Igunga Selwa Haji kwa lengo la kuwainua wananchi kiuchumi kwa kujiajili wenywe kupitia kazi za mikono yao wenyewe na kuacha utegemezi kutoka kwa waume, wake au ndugu na jamaa zao, amesema Maria Isdory Mwakilishi wa vijana Taifa  TWCC . 
 
Ameendelea kusema kuwa, amefundisha aina mbili za masoma ambayo ni somo la kutengeneza mafuta ya kujipaka ya mgando na sabuni ya kufulia nguo, ikiwa ni pamoja na matilio ambayo yanatumika kutengenezea bidha hizo, sheria na kanuni za usalama ili kujikinga na baadhi ya kemikali zinazotumika kutengeneza sabuni za kufulia. 

"kama mlivyoona hapo awali nimewafundisha vifaa ambavyo vinatumika kutengenezea bidhaa na jinsi ya kuvipata kwa urahisi, sheria na namna ya kujikinga na matumizi ya kemikali zinzaotumika kutengenezea sabuni, usafi binafsi kabla ya kuanza kutengeneza, namna ya kujisajili kupata vibali kutoka BRELA, Maendeleo ya Jamii, kupata nembo ya ubora kutoka TBS na wadau wengine kama hao," akisema Isdory. 

Kwa upande wake John Sollo Mwenezi wa kata ya Nanga kupitia CCM amewataka wananchi kujitokeza zaidi pindi wanaposikia fursa kama hizi za mafunzo ya bure ya ujasiliamali kwani ndio lengo la serikal ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia ya kumkomboa kiuchumi mwananchi kwa kuanzisha viwanda vidogovidogo. 

"Niwaombe tu wananchi wenzangu kutumia fursa adhimu kama hizi kujitokeza kujifunza namna ya utengenezaji wa sabuni, mafuta, usindikaji wa mazao ya chakula na kazi zingine za mikono, hii itatusaidia kujikomboa kiuchumi, pia Serikali kupitia Halmashauri zetu nchini, TASAF na Ofisi ya Waziri Mkuu imekuwa ikitoa mikopo kwa vikundi, wasiojiweza na wajasiliamali ili waweze kukuza bidhaa zao na mitaji yao jambo ambalo limesaidia vijana, wanawake, wazee na walemavu kujikomboa kiuchumi na hili ndilo lengo kuu la Serikali yetu sikivu, "  amesema Sollo. 

Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake kata ya Nanga Neema Abeli Mbogo, ametumia fursa hiyo kuwataka wanawake na vijana kuungana na kuanzisha vikundi vya ujasiliamali kwa lengo la kujiunga na majukwaa mbalimbali ya ujasiliamali ili waweze kupata uzoefu kutoka kwa watu wengine waliofanikiwa kupitia ujasiliamali na kazi za mikono kwani huwa wanafanya makongamano na maonyesho katika shughuli mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali. 

Huku wanufaika wa mafunzo hayo, Neema betura akisema kuwa, "Nashukuru kupatiwa mafunzo haya kwa vitendo ninatumaini sasa na mimi ninakwenda kuanza kutengeneza bidhaa hizi tulizo jifunza japo kwa kuanza kidogokidogo mpaka hapo ntakapo komaa na kuwa mzalishaji rasmi." 

"Nimpongeze mwalimu Maria kwa kujitoa kwake na kutujali sisi watu wa vijijini kwani hii ni fursa adimu sana kwetu, hivyo nimuombe atenge muda zaidi aje atufundishe kwa muda mrefu bidhaa mbalimbali kwani leo tumejifunza bidhaa mbili tu,"  amesema Bertha Richard.

Post a Comment

0 Comments