RAIS MWINYI: SMZ ITAENDELEA KUIIMARISHA SEKTA YA ELIMU


Na Mwandishi Wetu 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali vu Mwinyi amesema Serikali   itaendelea Kuimarisha Miundombinu ya Sekta ya Elimu kwani ndio Kipaumbele cha kwanza cha  Serikali anayoiongoza.

Rais Dkt. Mwinyi amesema hayo  wakati wa Ufunguzi wa Skuli Tatu Mpya za Msingi za Ghorofa za Chumbuni, Kidichi na Skuli ya Msingi ya Abeid Amani Karume  iliopo Mwera.

Aidha Rais Dkt.Mwinyi  amefahamisha kuwa Serikali inajikita  Kuimarisha Sekta ya Elimu kuanzia ngazi ya Msingi , Sekondari na Vyuo Viikuu  kwani ni nyenzo Muhimu ya kufanikisha Maendeleo katika Sekta zote.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi  ameeleza kuwa Serikali itaendelea na Ujenzi wa Skuli za ghorofa katika maeneo mbalimbali  pamoja na Kuongeza Idadi ya Walimu sambamba na Kuimarisha Maslahi Yao  ili watekeleze Majukumu Yao kwa Ufanisi zaidi.

Vilevile Rais Dkt.Mwinyi amefahamisha kuwa Serikali inakusudia kuzifanya Skuli zote kuwa na Viwango Bora vya kujifunzia kwa kuwa na Vifaa vya kutosha vya kujifunzia, Maabara, Maktaba na Vyumba vya Kompyuta Ili kuwaandaa Wanafunzi katika ngazi za awali.

Naye Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Lela Muhammed Mussa  amesema Mageuzi Makubwa yanayoendelea katika Sekta ya Elimu  yanasaidia  Kuongeza Ufanisi katika Utekelezaji wa Mtaala Mpya wa Elimu na Ongezeko la Ufaulu wa Wanafunzi.

Akiwasilisha Taarifa ya Kitaaluma ya Ujenzi wa Skuli hizo Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Khamis Abdalla amesema kila Skuli imegharimu Kiasi cha Shilingi Bilioni 4.5 hadi kukamilika zikiwa na Madarasa 29 kila Moja , Maabara, Maktaba na Vyumba vya Kompyuta.

Post a Comment

0 Comments