RAIS SAMIA AHUDHURIA HAFLA YA UAPISHO WA RAIS NDAITWAH WA NAMIBIA



*KAZIINAONGEA*

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amehudhuria hafla ya uapisho wa Rais wa Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah Machi 21, 2025. Sherehe hizo pia zinaambatana na maadhimisho ya miaka 35 ya Uhuru wa nchi hiyo ambapo Rais Dkt. Samia amealikwa kuwa Mgeni Rasmi katika sherehe hizo.

Aidha, Rais Samia aliwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako, Windhoek nchini Namibia mapema Machi 21, 2025 kwa ajili ya kuhudhuria hafla hiyo 

Namibia imeingia katika historia inayofanana na Tanzania kwa kupata Rais wa kwanza mwanamke kushika wadhifa huo nchini humo tangu ilipopata uhuru kutoka kwa Afrika kusini mwaka 1990.

Rais Nandi-Ndaitwah mwenye umri wa miaka 72, aliyeshinda kinyang'anyiro hicho, kwa kupata asilmia 57 ya kura, akiwa mgombea aliyetokea chama tawala cha SWAPO. 

*#Kazi na Utu, Tunasonga Mbele*

Post a Comment

0 Comments