RAIS SAMIA AIPAISHA TANZANIA KIMATAIFA KWENYE UONGOZI


#KAZIINAONGEA

Uwezo wa kiutendaji wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uongozi umeifanya Tanzania kuendelea kung'ara katika medani za uongozi wa Afrika.

Rais Dkt. Samia sasa anazidi kuthibitisha kuwa yeye ni kinara wa mabadiliko na yuko mstari wa mbele katika kusukuma ajenda ya wanawake katika uongozi wa bara hili.

Kwa mara nyingine, historia imeandikwa baada ya hivi karibuni kupewa heshima ya kuwa mgeni rasmi katika kuapishwa kwa Rais wa kwanza mwanamke wa Namibia, Netumbo Nandi-Ndaitwah tukio linalodhihirisha athari kubwa ya uongozi wake ndani na nje ya Tanzania.

Rais Samia, akiwa ndiye mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya Urais Tanzania, amekuwa kielelezo cha uthubutu, maono, na uthabiti wa wanawake katika uongozi.

Tangu aingie madarakani mwaka 2021 amebadili taswira ya uongozi wa kisiasa Afrika, akionyesha kuwa wanawake wanaweza kuongoza kwa ufanisi,
hekima, na weledi mkubwa.

Kwa sasa mataifa wanawake wengi wanafuata nyayo zake, huku Namibia ikifungua ukurasa mpya wa historia yake kwa kumpata rais mwanamke kwa mara ya kwanza.

Ushiriki wa Rais Samia katika hafla hiyo haukuwa wa kawaida na ni ishara kuwa Afrika inatambua mchango wake kama mwanzilishi wa enzi mpya ya uongozi wa wanawake.

Rais Dkt. Samia anaingia kwenye rekodi ya kuwa wanawake wachache duniani kubomoa ukuta uliowazuia wanawake kwa miaka mingi kufikia nafasi za juu za maamuzi.

Katika kipindi kifupi cha uongozi wake, Rais Samia ameimarisha diplomasia ya Tanzania, akiheshimika kote barani Afrika na duniani kwa kuongoza kwa vitendo na kuwa mfano bora, amewatia moyo wanawake waliokuwa wakihisi kwamba nafasi za juu za uongozi ni kwa ajili ya wanaume pekee.

Ushindi wa Netumbo Nandi - Ndaitwah ni ushindi wa wanawake wote wa Afrika.

*#Kazi na Utu, Tunasonga Mbele*

Post a Comment

0 Comments