SHAMIRA ACHANGIA UJENZI NYUMBA YA MTUMISHI MKOA WA MAGHARIBI, ZANZIBAR.



NA MWANDISHI WETU 

Mjumbe wa Baraza kuu UVCCM Taifa Viti Vitatu Tanzania Bara Ndg. Shamira Mshangama akiwa Zanzibar kwenye muendelezo wa ziara yake amefanya zoezi la ukaguzi wa nyumba ya Katibu wa UVCCM Mkoa wa Magharibi, Zanzibar.

Katika ziara yake hio ametembelea na kukagua ujenzi wa nyumba ya Katibu na kuchangia tipa 4 za kokoto kwa kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Magharibi  inayoongozwa na Mwenyekiti wake Ndg. Beshuu Juma Hamis.

Akiwa kwenye ukaguzi wa ujenzi nyumba hio ya katibu wa UVCCM mkoa wa ambayo iko katika hatua za mwisho. Amesisitiza kuwa pamoja na kazi zote tunazofanya lakini viongozi tunajukumu la kuzingatia ujenzi wa CCM na Jumuiya zake.

“Naamini nyumba hii ya Katibu wa UVCCM ikikamilika itaenda kupunguza baadhi ya gharama ambazo Jumuiya inaingia katika kumtafutia sehemu ya kuweka malazi Mtendaji wetu wa vijana mkoa wetu, pia sasa itakuwa ni rahisi kwa Jumuiya kujua ni wapi tunaweza kumpata Mtendaji wetu kwa haraka zaidi”. Ameongeza Mshangama

Post a Comment

0 Comments