NA MWANDISHI WETU, KIBAMBA
Aliyekuwa kiongozi wa Klabu ya soka ya timu ya Yanga Beda Tindwa hatimaye amejitosa kuchuhukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Kibamba lililopo Jijini Dar es Salaam.
Tindwa , amechukua fomu hiyo katika ofisi za chama cha mapinduzi (CCM) na kusema kwamba ameamua kuingia katika kinyang'anyoro hicho kwa lengo la kuweza kuketa mabadilikl kwa wananchi wa Jimbo la Kibamba.
Tindwa,amewahi kuwa Mjumbe wa kamati ya utendaji na Mjumbe wa kamati ya mashindano ya Klabu ya Yanga katika kipindi cha mwaka 2013 hadi 2022.
Zoezi la uchukuaji wa fomu katika kuwania nafasi mbali mbali linaendelea kushika kasi katika maeneo mbali mbali katika nafasi za udiwani na ubunge.
0 Comments