WAKILI MSOMI MACKDONALD LUNYILIJA AJITOSA UBUNGE JIMBO LA KINONDONI



NA MWANDISHI WETU

WAKILI Msomi Mackdonald Lunyilija amechukua Fomu ya kuomba ridhaa ya Chama chake kugombea Ubunge Jimbo la Kinondoni, Dar es Salaam

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 30, 2025 mkoani Dar es Salaam baada ya kukabidhiwa fomu hiyo, Lunyilija  amesema amechukua fomu hiyo kutimiza wajibu wake wa kidemokrasia.

Kwamba hii ni mara yake ya nne kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama chake ambapo alifanya hivyo mwaka 2010, 2015, 2020 na sasa 2025.

Lunyilija, amekabidhiwa fomu na Katibu wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Amos Richard.

Post a Comment

0 Comments