JAJI MWAMBEGELE ATEMBELEA GEREZA LA BUTIMBA KUSHUHUDIA UBORESHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA



NA MWANDISHI WETU

MWENYEKITI wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya Rufani MH.JACOBS MWAMBEGELE leo ametembelea Gereza Kuu la BUTIMBA la Mkoa wa Mwanza na kushuhudia mwenendo wa  Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa Mahabusu na Wafungwa wenye kifungo chini ya miezi  ikiwa ni siku moja kabla ya kuhitmisha zoezi hilo Julai 4, 2025.

Akizungumzia zoezi hilo kwa mikoa sita ya Kanda ya ziwa aliyotembelea na kushudia mwenendo wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Vituo vya Magereza vinbavyoshiriki mzunguko wa tatu katika awamu ya pili alisema utekelezaji wa zoezi hilo ni hitaji la takwa la kisheria ambayop imetoa ruhusa kwa Mahabusu na Wafungwa chini ya miezi sita kupiga Kura katika uchaguzi wa Oktoba Mwaka huu. 

Aidha, Mmoja  wa Watendaji wa Uboreshaji  wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kutoka Gereza Kuu la BUTIMBA lililopo jijini Mwanza anaeleza zoezi hilo linavyoendelea na namna lilivyo pokelewa. 

Kwa mujibu wa ratiba zoezi hilo la uboreshaji wa Dafatri kwenye Magereza na Vyuo vya Mafunzo linafanyika kwa siku saba, lilianza Juni 28 na linakamilika Julai 04, 2025.

Wanaohusika katika uboreshaji huo ni mahabusu, wafungwa  na wanafunzi wa vyuo vya mafunzo Tanzania Zanzibar ambao ni raia wa Tanzania walihukumiwa kifungo chini ya miezi sita.

Post a Comment

0 Comments