KAMPUNI YA LAZZIZ BAKERY YAJA NA KEKI YA KIPEKEE ILIYOPAMBWA MIRADI YA KIMKAKATI YA SERIKALI, nikatika maonesho ya 49 ya sabasaba, inauzito wa kilo 3000




NA MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya Lazziz Bakery imeibuka na ubunifu wa kipekee katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) kwa kutengeneza keki kubwa ya aina yake yenye uzito wa tani 3, sawa na kilo 3000 ikiwa imepambwa na miradi ya kimkakati iliyotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msimamizi Mkuu wa Lazziz Bakery, Saima Yusuf, amesema kuwa keki hiyo si ya kawaida bali imebuniwa kwa ustadi mkubwa kwa lengo la kuonyesha mandhari ya miundombinu muhimu ya Taifa. 

Ametaja miundombinu hiyo kuwa ni pamoja na Ikulu ya Tanzania, Shule, Reli ya Kisasa (SGR), majengo ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Barabara kuu pamoja na uwanja wa ndege wa kisasa.

Kwa mujibu wa Saima, ubunifu huo umeifanya keki hiyo kuwa kivutio kikubwa katika viwanja vya Sabasaba, huku wageni kutoka maeneo mbalimbali wakimiminika kutembelea banda la Lazziz Bakery kujionea ubunifu huo wa kipekee.

Hata hivyo amesema lengo la kuweka miradi hiyo katika keki ni kumpongeza Rais Dkt. Samia kwa kazi kubwa aliyofanya hususan katika kuhakikisha utekelezaji na ukamirishwaji wa miradi hiyo.

“Wote mnakaribishwa siku ya tarehe 7 Julai kushiriki tukio maalum la kukata na kula keki hii kubwa, ambapo huduma hiyo itatolewa bila malipo yoyote,” amesema Saima.

Post a Comment

0 Comments