MWENYEKITI CHAWATA KOMBOZA AJITOSA UBUNGE JIMBO LA KINONDONI



NA MWANDISHI WETU 

MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Walemavu Tanzania (Chawata) Hamad Komboza amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama kugombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 2, 2025 Komboza amesema amechukua fomu baada ya kupata msukumo kutoka kwa Wanachama wa Chawata wakimtaka achukue fomu hiyo.

Hata hivyo amesema pamoja na msukumo huo ni haki yake ya kikatiba kama Mwanachama wa CCM kujitokeza na kuomba ridhaa ya Chama.

Kadhalika amesema ameshawishika baada ya Rasi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alipokuwa akihutubia Bunge kuwahimiza na Walemavu kujitokeza na kuomba nafasi mbalimbali za kugombea.

Post a Comment

0 Comments