VETA YAJA NA MAJIKO YANAYOTUMIA NISHATI SAFI, lengo kuunga mkono kampeni ya Rais Samia ya matumizi ya nishati safi ya kupikia



NA ABRAHAM NTAMBARA

KATIKA kuunga mkono kampeni ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhamasisha Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imekuja na majiko maalum yanayotumia nishati hiyo.

Hayo yamebainishwa Julai 7, 2025 na Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore akikizungumza alipotembelea banda la VETA katika Maonyesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Kambarage Nyerere vilivyopo Barabara ya Kilwa Jijini Dar es salaam.

CPA Kasore amesema kuwa kwa sasa agenda kubwa inayozungumza ni suala la matumizi ya Nishai Safi ya Kupikia ambapo Rais Dkt. Samia ni Kinara katika kuhakikisha kila Mtanzania anatumia Nishati hiyo. 

"Sisi kama VETA tumekuja na eneo la utengenezaji wa majiko ambayo yanatumika kwenye maeneo yale makubwa ya kutumia watu wengi,Serikali ilielekeza Taasisi,na Mashirika ya Serikali na Binafsi yenye kulisha zaidi ya watu 100, kutoka kwenye matumizi ya mkaa nakuhamia kwenye matumizi ya Nishati Safi," amesema CPA Kasore

Amesema kuwa ili kuweza kufanikiwa agenda hiyo ya Serikali ya Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia lazima kuwepo na vifaa vinavyohitajika kuwepo, na kwamba VETA inatengeneza majiko yakuweza kutumika katika maeneo hayo.

"Kwahiyo tunawakaribisha kwa ajili ya kupata majiko lakini pia kuhakikisha kwamba ile sera na ile jitihada ambayo mhe. Rais amekua aki iishi katika matumizi ya Nishati safi na sisi tunaitekeleza nakuhakikisha wananchi wanatambua na wanakua na uwezo wa matumizi ya Nishati hiyo. 

Nakuongeza kuwa "Sambamba na hilo tunawakaribisha wananchi waje kwenye banda letu kuja kuaona vitu ambavyo VETA tunavifanya,tuna mageuzi makubwa sana, tumeyafanya katika Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi hapa Nchini, na sasa hivi  tunatoa ujuzi mwingi sana,kila eneo la ujuzi tunalo, hakuna eneo ambalo wewe utakuja utasema hujui."

Kwamba kwa sasa VETA pia  inatoa ujuzi wa wale watu wanaofanya kazi majumbani nakuweza kuhudumia wazee,nakwamba wanalo darasa ambalo wamehitimu karibu watu 700 na wapo kwenye ajira. 

"Tunapenda kumshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuweka msisitizo katika hii Elimu ya Amali(Ufundi stadi),ambao sisi kwetu VETA tumeona manufaa makubwa sana,na tumefaidika sana,na Rais ameweza kutekeleza mambo mengi sana,kwasasa tuna vyuo vya Veta 80 Nchini vinavyofanya kazi,na vipo vyuo 65 ambavyo Serikali inaenda kuvimalizia."amesema

Aidha amesema kuwa Rais Dkt. Samia ametoa takribani bilioni.100 kwa ajili ya ujenzi huo na ujenzi upo katika hatua nzuri katika ukamilishaji wa awamu ya kwanza,hivyo VETA itakua na jumla ya vyuo 145 hapa nchini,ambapo kila Wilaya hapa nchini itakua na chuo Cha Ufundi Stadi. 

Amehitimisha kwa kuongeza kuwa Vyuo hivyo  vinaenda kusaidia wananchi kuweza kupata urahisi wa elimu na ujuzi ambao wanauhitaji,lakini pia lengo la vyuo hivyo ni kuhakikisha mafunzo yanatolewa kulingana na shughuli za kiuchumi na shughuli za kijamii zinazo fanyika katika kila Wilaya. 

Post a Comment

0 Comments