VIJANA WAZIDI KUVUTIWA NA UTENDAJI WA RAIS SAMIA, wajitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kugombea uongozi akiwemo Elia Mathayo Kwangu




#KAZIINAONGEA

Vijana nchini wameendelea kuonyesha mwitikio mkubwa katika kushiriki uongozi baada ya kuvutiwa na uongozi wa Rais Samia kupitia falsafa zake za R4, hususani katika kipindi hiki cha uchukuaji fomu za kugombea nafasi za Ubunge na Udiwani kilichoanza rasmi Juni 28, 2025.

Mmoja wa vijana waliovutiwa na uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni Elia Mathayo Kwangu, ambaye ameonesha nia ya kugombea nafasi ya Udiwani katika Kata ya Kitunda. Elia amesema kuwa utendaji wa Rais Samia umemhamasisha kujitosa kwenye uongozi ili kushirikiana naye katika kuendeleza jitihada za maendeleo zinazotekelezwa nchini.

“Nimeguswa na dhamira ya dhati ya Rais Samia ya kuimarisha maendeleo ya wananchi kwa kusikiliza, kushirikisha, kupatanisha na kuweka mbele maslahi ya Taifa. Ninaamini vijana tuna nafasi kubwa ya kusaidia juhudi hizi katika ngazi za chini,” amesema Kwangu.

Zoezi la uchukuaji fomu linaendelea na linatarajiwa kufungwa rasmi Julai 2, 2025, saa 10:00 jioni. Mwitikio mkubwa wa vijana unaashiria ongezeko la hamasa ya kizazi kipya kushiriki katika siasa na uongozi wa Taifa kwa maendeleo endelevu. 

Post a Comment

0 Comments