NA MWANDISHI WETU
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka Waumini wa madhehebu mbalimbali ya dini kuwa baraka kwa wengine kila mahali wanapokuwa ili kusababisha furaha kwa sababu yao.
“ Wewe geuka kuwa chumvi ya ulimwengu, Chumvi iko kila nyumba ndiyo maana Yesu hakusema nyinyi ni sukari ya Dunia kwa sababu Sukari inamaringo, Sukari ipo kwenye nyumba za matajiri tu lakini chumvi ipo kila nyumba, hakuna masikini ambaye ndani ya nyumba yake hakuna chumvi, basi na ninyi nendeni mkawe chumvi ya watu wengine”.
Dkt. Biteko amesema hayo Agosti 12, 2025 wakati akimwakilisha Mheshimiwa Rais katika Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 40 ya Kuzaliwa kwa Dayosisi ya Kagera iliyofanyika katika Viwanja vya Kanisa Kuu Yohana Mbatizaji – Murgwanza, Ngara.
“ Nenda ukawe baraka kwa wengine kwa nafasi ndogo ulionayo au kubwa ulionayo, ukifanya hivyo wakati watu wanamshukuru Mungu kwa ajili yao basi na wewe utabarikiwa”.
0 Comments