ADO AKUTANA NA WADAU WA SEKTA YA MADINI TUNDURU



Mbunge wa Tunduru Kaskazini Ndugu Ado Shaibu Ado amekutana na wadau wa sekta ya madini Tunduru ikiwemo Maofisa wa Ofisi ya Ofisa Mgodi Mkaazi Tunduru, wanunuzi wa madini, madalali, wadhamini na wachimbaji wa madini kwa ajili  ya kujitambulisha na kusikiliza changamoto zao. 

Kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Klasta Tunduru Mjini leo tarehe 7 Desemba 2025 ni mwendelezo wa ziara ya Mbunge wa Tunduru Kaskazini kukutana na wadau wa maendeleo ikiwemo upande wa Serikali, makundi mbalimbali ya kijamii na wananchi kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments