Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam
Ubalozi wa Kenya na Marekani uliopo nchini umeombwa kuwarejesha wanaharakati wote akiwemo Mange Kimambi na Maria Sarungi waliohusika kuwashawishi watu Kupitia mitandao ya kijamii kufanya maandamano yasiyo na kibali Oktoba 29,2025 siku ya Uchaguzi Mkuu na kusababisha madhara Makubwa vifo na kuribiwa Mali.
Wito huo umetolewa Leo Desemba 17 Jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Kituo cha Wanahabari Watetezi wa Rasilimali za Taifa ((MECIRA) Habibu Mchange ambapo Amesema tayari wameshawasilisha barua katika Balozi hizo ili zifanyiwe kwani hao hao watanzania waliohamia ardhi za Nchi hizo mbili wametumia mitandao ya kijamii kuchoche Vurugu ili kuivuruga tunu ya Amani iliyokuwepo
"Watanzania tushirikiane na tupaze sauti kuiambia dunia kwamba tunafahamu kinachoendelea , Marekani ieshimu uhuru na mamlaka ya Tanzsnia, tunaweza kujiendesha na tunafahamu yupo muhalifu ambaye ni Mange Kimambi amejificha katika ardhi Yao tunatambua wao wanapambana na wahalifu na mhalifu mmojawapo ni Mange yupo kwenye ardhi yao, wamrudishe kwakuwa amekuwa sehemu ya kuchochea vurugu nchini"amesema Mchange
" Kwani Mange amekiri kwamba kitendo cha meta kuzuia akaunti zake kimekwamisha kuzuia vurugu za Disemba 9 ,2025 pia amewashukuru wakenya na kusema waendelee kuwasaidia kama wanavyowasaidiaga kwa maana tunajua wanaowatunza hao akina HildaNewton wapo Kenya na wanahusika na machafuko..tunaitaka Kenya na wao kutoa ushirikiano wao katika kuwakamata ikiwemo Maria Sarungi "
Mchange amesisitiza Kwa kusema ikitazamwa Kwa undani hao wote waliochochea hizo vurugu na kuendelea kuchochea ni wanaharakati wa hovyo ambao hawaishi nchini ndio maana sisi kama MECIRA wamelitoa manga kiziandika barua balozi za Marekani na Kenya kuwataka kuwarudishia hao watu kwakuwa wanaishi kwenye ardhi zao
Aidha kituo hicho kimewahimiza wanahabari, wanaharakati na wananchi kwa ujumla kutumia kalamu, majukwaa ya mawasiliano na mitandao ya kijamii kwa njia chanya inayojenga jamii badala ya kubomoa mshikamano wa kitaifa na kikanda
0 Comments