MBETO AMPASHA OMO WAZABZIBARI WAMECHOSHWA NA MAISHA YA HASAMA


Na Mwandishi  wetu , Zanzibar 

Cha Mapinduzi  kimemtaka Mwenyekiti  wa ACT Wazalendo  Othman  Masoud  Othman kuacha porojo na kuwapotosha wananchi kwa kupandikiza maneno  ya hasama na  chuki  katika jamii huku akiahidi mambo  yasiowezekana.

Vile vile,  CCM kimesisitiza kuwa Uchaguzu  Mkuu umeshamalizika, wananchi  wametumia haki yao ya  kikatiba na kidemokrasia kwa kuiweka Serikali  walioitaka  madarakani.

Matamshi  hayo yametamkwa na Katibu wa Kamati  Maalum  ya NEC  Zanzibar, Idara ya itikadi, Uenezi  na Mafunzo, Khamisi  Mbeto Khamis aliyemtaka Othman kukubali ukweli    ameshindwa  Uchaguzi kutokana na nguvu ya maamuzi ya wengi.

Mbeto  alisema  Othman hana sababu zenye mashiko ,bali  anajaribu  kuidanganya dunia akidai  yeye ndiye mshindi wakati Tume  ya Uchaguzi  Zanziabr  imeshamtangaza mgombea aliyeshinda Urais  .

Alisema Othman  asingeweza kumshimda mgombea wa CCM Rais  Dk Hussein  Ali Mwinyi   kwa sababu kadhaa muhimu  ambazo   zina ukweli usiokwepeka.

'Othman alikuwa akiomba  nafasi y kuchaguliwa  ili awatumikie wananchi wa Zanziabr. Rais  Dk  Mwinyi alishapimwa jinsi  ilivyoitumikia  nchi na watu  miaka mitano iliopita.  Ndoto  ya OMO ni  kuleta  Maendeleo wakati mwenzake alishafanya kazi  ya kuleta   maendeleo inayoonekana"  Alisema Mbeto


Aidha,  Katibu  huyo Mwenezi  alisema fikra na hesabu za Othman ? alidhani wananchi  wangembagua na kumchukia  Rais Dk  Mwinyi kutokana na matamshi ya Makamu wake Mwenyekiti  Ismail Jussa Ladhu alivyokuwa akitumia hutuba za  ubaguzi kama sera na mtaji wa kupata  ushindi.

"Zanzibar  nchi ya Visiwa. Ni mkusanyiko na mkutanisho wa watu toka pembe nyingi  za  dunia .Unapoonyesha au chama chako kina sera za  kibaguzi unalazimisha upigiwe   kura za chuki  dhidi yako" Alieleza 

Pia Mwenezi huyo alisema miaka mitano iliopita utawala wa  Rais  Dk Mwinyi,  umewaunganisha wananchi  waliogawanyika kwa siasa za chuki .Ameongoza bila kujali  asili zao ,rangi walizonazo ,Siasa au itikadi  za vyama vyao.

"Ka miakaa mitano iliopita  Wazanzibari  waliishi kwa utulivu kama maji ndani  ya mtungi. Wamekuwa wamoja ,wenye  upendo mshikamano. Hazikusikika sauti za kubaguana, kusimangana wala kuhitilafiana "Alisisitiza 

Mbeto alimtaja kiongozi  pekee  ambaye  kila wakati alisikika  katika mkutano  yake akijaribu kuwagawa wananchi  asili,nasaba na siasa ili kuwavuruga kwa historia na   matukio ya kisiasa yaliopita ni Jussa peke yake. 

"Kushindwa kwake OMO kwa sehemu kubwa kumeporomoshwa na aina ya utata wa   Siasa na matamshi ya Jussa. Wazanzibari wamwchoshwa na heka heka za kubaguana na kugombanishwa kwa itikadi za vyama"Alisema Mwenezi huyo.

Post a Comment

0 Comments