MBETO: RAIS DK MWINYI KUIACHIA ZANZIBAR MAENDELEO YA MFANO DUNIANI


Na Mwandishi  Wetu, Zanzibar  

Chama Cha Mapinduzi kimesema Uongozi katika ngwe ya pili  chini ya  Rais Dk Hussein Ali Mwinyi utaiachia Zanzibar  alama zisizofutika kwa Maendeleo  ya Nchi na Watu wake.

Alama na zawadi hizo zitabaki kuwa kumbukumbu zisizofutika miaka na miaka kwa maendeleo ya za Zanzibar .

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar , Idara ya  itikadi, Uenezi na Mafunzo,  Khamis Mbeto  Khamis,  ameeleza hayo mbele ya Waandishi wa Habari Ofisi kwake Kisiwandui Mjini Unguja. 

Katika maelezo yake, Mbeto  aliitaja Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kisasa huko Pemba na Barabara ya lami ya njia Nne  toka Chake Chake hadi Mkoani yenye Umbali wa Kilomita 45.3 Mkoa wa Kusini Pemba. 

Kadhalika Mbeto  alisema utafanyika  Ujenzi wa Uwanja mkubwa wa Soka ambao  utatumika katika Michuano ya Afcon , unaochukua Watazamaji zaidi  ya 40 elfu huko Fumba Mkoa wa Mjini Magharibi.

Pia akataja  kuna Ujenzi  wa Barabara  toka  Tunguu - Makunduchi  hadi Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja wenye Umabli wa kilomita 47.

"Sera za CCM chini  ya SMZ katika uongozi  wa Rais Dk Mwinyi utaacha alama za kudumu. Alama hizo zitabaki  kuwa  kumbukumbu muhimu  kwa  maendeleo  ya wazanzibari wote " Alisema Mbeto 

Aidha, akiitaja Miradi mingine ,alisema ni Ujenzi  wa Bandari ya Abiria huko Maruhubi kwa Mpigaduri na Ujenzi wa Nyumba za Makaazi ya Watu za  Kisiasa za wakaazi elfu kumi   Unguja na Pemba.

"Kutakuwa na  Usafiri wa mfumo wa   Mabasi ya Kisasa ya Abiria na watalii  katika Mji wa Unguja .Pia zitajengwa treni zitakazopita kwenye  barabara za lami. Ujenzi wa  Barabara ya lami inayounganisha Mkoa wa Mjini na Kaskazini Unguja toka   Kinazini hadi Bububu "Alieleza Mwenezi  huyo.

Akifafanua zaidi,akisema kuna  Mradi wa Uzalishaji wa Umeme utakaomaliiza kero hiyo kwa Zanzibar ,hospitali ya kufundishia  ya  kisasa na Chuo Kikuu cha  Afya kitakachojengwa Binguni Mkoa wa Kusini Unguja .

"Serikalii chini  ya Utawala wa Rais  Dk Mwinyi utaacha  alama zisizofutika  Unguja na Pemba . Atakapoondoka madarakani  atakumbukwa kwa kuitumikia nchi na watu wake  " Alieleza Mbeto.

Post a Comment

0 Comments