NA MWANDISHI WETU, LONGIDO
Baraza la Wafanyakazi la Halmashauri ya Wilaya ya Longido leo Februari 18, 2026 limepitisha rasimu ya mpango na bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 yenye makisio ya jumla ya shilingi bilioni 41,287,492,000.00 kwa ajili ya matumizi ya kawaida (OC), mishahara (PE) na miradi ya maendeleo.
Akiwasilisha rasimu hiyo katika Mkutano Maalum wa Baraza la kujadili mapendekezo ya mpango na bajeti ya Halmashauri kwa mwaka 2026/2027, uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri J.K Nyerere, Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo, Bw. Innocent Mariki, amesema kiasi hicho kinatarajiwa kupatikana kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato.
Akifafanua mgawanyo wa bajeti hiyo, Bw. Mariki amesema shilingi bilioni 5,487,126,000.00 sawa na asilimia 13.29 ni mapato ya ndani, shilingi bilioni 1,407,368,000.00 sawa na asilimia 3.41 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida, shilingi bilioni 17,819,784,000.00 sawa na asilimia 43.16 ni kwa ajili ya mishahara, na shilingi bilioni 16,573,214,000.00 sawa na asilimia 40.14 zimetengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Kuhusu makisio ya mapato ya ndani, amesema Halmashauri inatarajia kukusanya shilingi bilioni 5,487,126,000.00 kutoka katika vyanzo vyake vya mapato. Makisio hayo yametokana na tathmini ya kina ya vyanzo husika kwa kuzingatia uwezo wa kila chanzo pamoja na mwenendo wa ukusanyaji wa mapato katika miaka mitatu iliyopita ya fedha (2023/2024, 2024/2025 na 2025/2026).
Akizungumzia matumizi ya kawaida kwa mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2026/2027 (halisi na lindwa), Bw. Mariki amesema Halmashauri inakisia kutumia jumla ya shilingi bilioni 4,749,274,800.00 kwa ajili ya shughuli mbalimbali za uendeshaji.
Aidha, Halmashauri inatarajia kutumia shilingi 737,851,200.00 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa fedha za mapato ya ndani, pamoja na shilingi bilioni 1,407,368,000.00 kwa ajili ya ruzuku ya matumizi mengineyo.
Kwa upande wa mishahara, Halmashauri inakisia kutumia shilingi bilioni 17,819,784,000.00 kulipa watumishi wake katika mwaka wa fedha 2026/2027.
.jpg)
0 Comments