NA MWANDISHI WETU, MBEYA
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Solomon Itunda amempongeza kwa dhati Mkurugenzi mtendahi wa Halmashauri ya Mbeya Bi. Erica Yeggela kwa juhudi zake za kushirikiana bega kwa bega katika kuleta mabadiliko chanya katika ongezeko la ukusanyaji wa mapato kwa kiwango cha zaidi ya asilimia zipatazo 75.
Itunda ameyasema hayo wakati wa kikao cha baraza la madiwani kilichohudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na chama chenye lengo la kuweza kuijadili masuala mbali mbali ya kimaendeleo na kuweka mikakati kabambe ya kusimamia miradi ya maendeleo pamoja ukusanyaji wa mapato kwa maslahi mapaaana ya wananchi.
"Mkurugenzi wangu nakupongeza sana tena sana kwa kuwa unafanya kazi nzuri na unashirikiana na watendaji wako vizuri na hii ndio inachangia kwa kiasi kikubwa katika kuifanya Halmashauri ya Mbeya iweze kuwa na maendeleo katika nyanja mbali mbali hasa katika ukusanyaji wa mapato ambayo yamepaanda hadi kufikia asilimia 75 hongera sana,"amesema Itunda.
Pia ameupongeza uongozi mzima wa Halmashauri ya Mbeya kwa kuweza kujipanga vizuri na kufanikiwa kushika nafasi ya kwanza ngazi ya kanda na kushika nafasi ya tatu kitaifa katika sherehe za kilele cha uzimaji wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa kwa mwaka wa 2025.
Kadhalika amemshukuru kwa kuweka mipango madhubuti kwa ajili ya kuweza kuwasaidia watoto wa shule za msingi na sekondari kupata chakula chha mchana lengo kubwa ikiwa ni kuoongeza kasi ya ufaulu kwa wanafunzi.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendahi wa Halmashauri ya Mbeya Bi. Erica Yeggela amemshukuru na kumpongeza Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuwajali wananchi wake kutokana na kutenga fedha nyingi amabzo zimekwenda kutekeleza miradi mbali mbali ambayo imekuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi kupata huduma mbali mbali kwa urahisi.

0 Comments