ESG kuwa Kipaumbele kwa Watumishi Wizara ya Madini na Taasisi zake, kuweka matumizi nishati Safi.




●Kupunguza uzalishaji 
   hewa ya ukaa
●Kuhakikisha Usalama 
   Kazini.
●Uwazi wa taarifa za 
  kifedha.

Dodoma

Watumishi wa Wizara ya Madini na taasisi zake wametakiwa kuzingatia viwango vya Kijamii, Mazingira na Utawala(ESG) katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ili kuimarisha uwajibikaji, uendelevu na utawala bora katika Sekta ya Madini nchini.

Wito huo umetolewa leo Februari 27, 2026 na Kamishna wa Madini Dkt. AbdulRahman Mwanga  wakati akifunga mafunzo maalum yaliyolenga kuwajengea uwezo watumishi kuhusu umuhimu wa kulinda mazingira , kuheshimu masuala ya kijamii na kuzingatia misingi ya uwazi na maadili katika utendaji kazi.

Dkt.Mwanga amesema kuwa, utekelezaji madhubuti wa kanuni za ESG utasaidia kuongeza imani ya wawekezaji , kulinda maslahi ya jamii zinazozunguka maeneo ya migodi na kuhakikisha rasilimali za madini zinatumika kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. 

Dkt.Mwanga amefafanua kuwa mojawapo ya kigezo cha uwekezaji ni suala la utunzaji wa mazingira kwa jamii hivyo  mafunzo haya yamewapa uelewa mpana kuhusu umuhimu wa tathimini za athari za mazingira , ushirikishwaji wa wadau pamoja na kuzingatia misingi ya maadili na uwajibikaji katika maamuzi ya kiutendaji.

Ameeleza kuwa, kwa kuzingatia viwango vya ESG mafunzo haya yanakuwa sehemu ya mkakati wa kuiwezesha sekta ya madini kuchangia kikamilifu maendeleo ya uchumi wa taifa kwa njia endelevu inayokubalika kimataifa.

Akizungumza kwa niaba ya waandaaji wa mafunzo hayo, Mratibu wa Mafunzo ambaye pia ni Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Madini CPA. Pili Kamali amesema kuwa moja ya malengo ya mafunzo ni kuhakikisha watumishi wanaandaa na kuwasilisha taarifa za fedha kwa kuzingatia misingi ya ESG  unasaidia kuongeza uwazi , uwajibikaji na uaminifu katika usimamizi wa rasilimali madini.

Kamali amefafanua kuwa  uandaaji wa taarifa za fedha unahusisha misingi ya ESG hususan katika kuzingatia athari za mazingira, kijamii na kiutawala kwa kufuata maelekezo ya Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi(NBAA).

Post a Comment

0 Comments