MAWAZIRI WA MAMBO YA NDANI TANZANIA NA ZAMBIA WATUA EDEN YA NGORONGORO NA UJUMBE WA WATU 170




Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro jana tarehe 26 Februari 2026 limepokea ugeni mzito uliongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa Tanzania, Mhe. Patrobas Paschal Katambi na Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Jacob Jack Mwiimbu pamoja na ujumbe wa wageni 70  wa majeshi ya ulinzi na usalama waliopo nchini kwa majukumu mbalimbali na kufanya utalii hifadhi ya Ngorongoro.

Waheshimiwa mawaziri na Ujumbe wao waliopata fursa ya kutembelea vivutio vilivyopo Ngorongoro na kushuhudia Wanyama wakubwa watano (Simba, Chui, Nyati, faru na Tembo), makundi ya Pofu, pundamilia, swala, Nyumbu, Ngiri, Viboko, ndege, mimea ya asili, kasoko ya Ngorongoro na kupata simulizi mbalimbali kuhusu utalii wa miamba na hadhi tatu za kitamaifa zilizopo Ngorongoro.  

Mhe. Katambi ameipongeza Ngorongoro kwa uhifadhi unaozingatia usalama wa mazingira, kulinda fahari ya Ngorongoro kama kivutio bora cha utalii Afrika.

Post a Comment

0 Comments