MBETO ASIFU UWEZO WA CCM KUJENGA TAASISI MAKINI YA KISIASA


Mwandishi  Wetu, Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi  ( CCM) kimesema wakati ifikapo Februari 5 Mwaka huu kitafikisha Miaka 49 toka kuzaliwa kwake Mwaka 1977, kinajivunia juhudi za  kufikia shabaha na malengo ya kuundwa kwa chama hicho  .

Vile vile  CCM kimesisitiza kitaendelea kusimamia  misingi ya Sera zake kwa kuendelea  kuhubiri tija na  faida ya  ustawi wa Amani ,Umoja na Mshikamano wa kitaifa .

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi ,Uenezi na Mafunzo,  Khamis  Mbeto  Khamis ameeleza hayo  akiwa Afisi Kuu ya CCM  Kisiwandui .

Mbeto  alisema kwa Miaka 49 Serikali  za CCM  zimemfanya  Mtanzania atoke katika  kadhia ya unyonge wa kunyonywa, kunyanyaswa  na kudharauliwa hadi kuwa  mtu huru  anayeheshimika. 

Alisema  CCM katika kuamini  Umoja wa Afrika, kimeshiriki kikamilifu katika harakati  zilizoleta Ukombozi wa Mataifa mengine Kusini mwa Afrika na sasa yako  huru.

"Kwa  miaka  49 Sera za  CCM zimemuweka mbali   Mtanzania na  maadui  Ujinga,Umasikini na Maradhi. Tunaelewa  maadui hao ni kazi  kumalizika kwa pamoja .Mapambano  dhidi yao  yataendelea"  Alisema Mbeto 

Aidha  alisema umadhubuti wa CCM  utabaki katika  kuziunganisha jamii  , kufuta   aina  zote za   unyonyaji, maonevu au  jaribio lolote la  kudhoofisha uchumi na kuzorotesha Maendeleo .

"Kuwepo kwa   Vituo vya Afya, Zahanati na  Hospitali  ni kumkabili adui  Maradhi. Kujenga   Shule za Msingi na Vyuo Vikuu ni mkakati wa  kufuta Ujinga. Miradi ya  Kilimo  ,Uvuvi, Ufugaji, ujenzi wa Viwanda, Barabara na Masoko  ni kumfanya kila mtu ajijenge kiuchumi" Alisema Mbeto  

Akizungumzia  ustawi wa maendeleo  ya  demokrasia ndani ya CCM, Mbeto  alisema  ushiriki wa wanachama katika kuamua  ,kuchagua na kuchaguliwa ,ni kielelezo cha kukomaa kwa tasisis  hiyo.

'Kwa miaka 49 tumejenga  taasisi  imara, makini  inayoaminiwa na kutegemewa na  Wananchi wote. Pia  Sera na Miongozo  ya  chama  chetu  imekuwa ikibadilka kulingana  na mahitaji ya nyakati" Alieleza

Post a Comment

0 Comments