MBETO: TUTASIMAMIA SHABAHA NA MALENGO YA ASP ZBAR

Na Mwandishi  Wetu, Zanzibar 


Chama Cha Mapinduzi kimesema serikali ya Awamu ya Nane Zanzibar chini ya Rais Dk Hussein Ali Mwinyi utasimamia Sera za CCM na kuendeleza  shabaha ziliowekwa na ASP kabla na baada ya Mapinduzi. 

CCM kimesisitiza pamoja na  kutunga Sera na dira ya Maendeleo ,hakitasahau kusimamia mkakati wa  vyama vya TANU na ASP .

Hayo yameelezwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC  Zanzibar, Idara ya Itikadi , Uenezi na Mafunzo,  Khamis Mbeto Khamis akitaja  nia ya SMZ ni  kuendelea na mpango   wake mkakati wa kujenga Nyumba mpya za Kisasa.

Mbeto  kwanza  alipongeza  uamuzi wa Wananchi Wakaazi  waliokuwa wakiishi  Nyumba  za Mjerumani zilizopo Kiwajuni Wilaya ya Mjini  ,kwa  kupisha Ujenzi wa Nyumba za Kisasa za Maghorofa uendelee.

Alisema malengo ya ASP  kabla na baada ya Mapinduzi ,yalikuwa ni  kuinua hali za Maisha ya jamii  kiuchumi , kuwapatia Makaazi bora,  kuimarisha huduma za Afya, Maji  Safi ,matibabu na kufikishia Nishati ya Umeme.

"CCM ni zao la TANU na ASP . Vyama hivyo  viliahidi ikiwa vitashika Dola. Kinachoendelezwa na  Rais Dk Mwinyi ni  Utekelezaji wa Sera za CCM na kusimamia shabaha za Vyama vya Ukombozi "Alisema Mbeto.

Aidha, Katibu  huyo Mwenezi aliongeza kusema  ni haki ya kila Mtanzania kupata Makaazi ya uhakika, huduma bora za  kijamii kama Afya , Elimu ,Makaazi , Usalama na Amani. 

"CCM kitatekeleza Sera zake za msingi kwa kusimamia na kutekeleza  shabaha za vyama vya ukombozi. Sera za CCM  zitaibadilisha Zanzibar na kuwavutia  Wawekezaji kuja na kuwekeza miradi mikubwa ya  kimaendeleo "Alieleza

Alisema  mara tu utakapokamilika Mradi wa Ujenzi  kwa  Nyumba za kisasa kwa  Mjerumani ,Kazi  hiyo  itafanyika katika nyumba za  Kilimani ikiwemo kujengwa  nyingine katika maeneo ya Mashamba .

"Maendeleo yatafike  Mjini na Mashamba .Kutajengwa  makaazi ya   kisasa, Shule ,Madaraja  na Masoko  Mjini na Mashamba"Alisisotiza . 

Pia Mbeto alisema Serikali Awamu ya  kwanza ilijenga  nyumba za kisasa Michenzini na Kilimani . Nyingine zikajengwa   Bambi, Mkwajuni, Mkokotoni na Makunduchi kwa Unguja"Alisema

Hata hivyo alisema Nyumba kama hizo pia zilijengwa  huko Pemba  maeneo ya  Mkoani, Wete, Micheweni, Kengeja  na Chakechake.

Post a Comment

0 Comments