TRA PWANI HAWANA BAYA YAWATHAMINI WATOTO YATIMA NA MAKUNDI MAALUM KWA IFTAR




NA VICTOR MASANGU, PWANI

Mamlaka ya mapato (TRA) Mkoa wa Pwani katika kurudisha fadhila kwa jamii imeamua kuandaa Iftar maalumu kwa ajili ya kufuturisha makundi mbali mbali ikiwemo watoto yatima, viongozi wa madhehebu ya dini, viongozi wa serikali ikiwa pamoja na wananchi kutoka maeneo ya Mkoa wa Pwani.

Tukio hilo  maalumu la Iftar limefanyika katika viwanja vya nje ya Ofisi ya TRA na kuongozwa na Sheikh wa Mkoa wa Pwani Khamis Mtupa pamoja na kuhudhuliwa na viongozi wengine wa dini pamoja na watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kutoka kituo cha Fadhila kilichopo kata ya Misigusugu Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha.

Katika  tuki hilo Sheikh wa Mkoa wa Pwani Khamis Mtupa ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi hakusita kuupongeza kwa dhati uongozi mzima wa TRA Mkoa wa Pwani kwa kuamua kurudish fadhila kwa jamii na kukusanya makundi mbali mbali ikiwemo watoto yatima na kula nao chakula cha jioni ikiwa ni moja na nguzo muhimu sana hasa katika kipindi hiki  cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

"Kwa upande wangu mimi kipekee nipende kuchukua  fursa hii kuwashukuru kwa dhati uongozi mzima wa TRA pamoja na meneja wake kwa kuona umuhimu mkubwa wa kutukutanisha siku ya leo katika hili tuko la Iftari kwa kweli mmefanya jambo la msingi sana na kingine nimependa mmekusanya makundi tofauti ikiwemo na watoto yatima ambao tumejumuika nao hapa katika tukio hilo na Mungu awabariki sana na muendelee na moyo huu wa kujitolea,"amebainisha Sheikh Mtupa.

Pia katika hatua  nyingine amebaainisha kwamba katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadani taasisis na watu mbali mbali wanapaswa kufanya matendo ya huruma kwa wahitaji ikiwemo suala la kuwafuturisha watu    wenye uhitaji na kuweza kutoa misaada mbaali mbali ambayo itaweza kuwasaidia walengwa na kwamba zoezi hilo liwe endelevu ikiwemo kusaidia jamii.

Kadhalika Sheikh Mtupa ameipongeza TRA Mkoa wa Pwani kwa kuweka mikakati madhubuti ambayo imeweza kusaidia kwa kiassi kikubwa katika suala zima la kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ambayo yanapelekea kuleta mabadiliko makubwa katika maendeleo kwa wananchi.

Kwa   upande wake Meneja wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Pwani Masawa Masawa amesema kwamba wameamua kufanya tukio la Iftar hiiyo na kuwakutanisha makundi mbali mbali ikiwa ni moja ya kurudisha fadhila kwa jamii pamoja na kukutana na watoto yatima na kula nao chakula cha jioni.

Meneja huyo amesema kwamba lengo kubwa la TRA Mkoa wa Pwani ni kuendelea kushirikiana begaa kwa bega na jamii katika mambo mbali mbali ikiwemo kukutana kwa pamoja na kubadilishanaa mawazo pamoja naa kula cha jioni kwani ni moja ya kuongeza wigo mpana ya katika kujenga mahusiano mazuri kwa jamii.,

Nao baadhi ya watoto yatima ambao wamehudhulia      katika tukio hilo  wamesema wamefurahishwa na uongozi  mzima wa TRA kwa kuweza kuwakumbuka katika kuwakutanisha katika Iftar hiyo na kusema kwamba wamejisikia furaha na amani ya kukutana na jamii nyingine.

Post a Comment

0 Comments