VIGEZO VINNE VYA KUMPATA MREMBO WA KIHADZABE, KARIBU JIOPAKI YA NGORONGORO





NA MWANDISHI WETU

Wahadzabe ni kabila linalopatikana pembezoni mwa ziwa Eyasi na habari za maisha yao zimehifadhiwa makumbusho ya Urithi Jiopaki liyopo Karatu.

Baadhi ya vidume vinatamani kuwaoa wasichana wa kihadzabe  lakini kuwapata si kazi rahisi, lazima utumize vigezo vinne kama ifuatavyo; 

Kwanza Usitahiriwe , Kabila hili linaamini kwamba mwanaume kutahiriwa hupunguza utaalam wa mambo na kufanya  mwili wako kuwa legelege.

Pili, uwezo wa kula Mizizi , matunda na nyama pori, wakiamini kuwa vitu hivyo hukupa nguvu ya kutosha na Jembe la kazi wakati wa tendo la ndoa na huitaji kutafuta Vumbi la Congo kama wala Chipsi mjini.

Tatu uwezo wa kulenga shabaha, wakiamini kwamba hutamlaza njaa  kila siku utarudi na nyama pori ambayo ni chakula hapo nyumbani.

Nne usiwe na mchepuko , wakiamini mtu anayechepuka anaweza kuuawa wakati wowote akifumaniwa kwa kuzini na pia kuleta maradhi nyumbani.

Karibuni makumbusho ya  Jiopaki na eneo la  ziwa Eyasi kwa wahadzabe ujue kuwa mcheza kwao hutuzwa

Post a Comment

0 Comments