MBETO: DUNIA HAINA SHAKA NA AINA YA DEMOKRASIA YA TANZANIA



Na Mwandishi  Wetu, Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi  kimejigamba kuwa Tanzania  inafuata na kutekeleza aina bora  ya demokrasia   chini ya uongozi wa   CCM , kutokana na upana wake,  ushiriki wa Wananchi  na Uwazi usiotiliwa  shaka. 

Pia chama hicho  kimesema kiwango cha ukosoaji, michango, fikra na maoni  jumuishi ya Wananchi  husikilizwa ,  kutekelezwa na medani za utawala .

Hayo yametamkwa na Katibu wa Kamati  Maalum  ya NEC  Zanzibar,Idara ya Itikadi, Uenezi  na Mafunzo , Khamis Mbeto Khamis  aliposhiriki   Mdahalo wa Muungano  ulioandaliwa na  Chuo Kikuu  cha Taifa SUZA kupitia Kigoda cha Taaluma cha Sheikh Abead Amani Karume.

Mbeto  alisifu uwamuzi wa Viongozi wa Mataifa ya Tanganyika na Zanzibar  kwa kutanguliza kwao maslahi mapana ya Taifa kwa kuwaunganisha Wananchi   Miaka  62 iliopita.

Aidha alisema kiwango cha  aina ya demokrasia iliopo nchini,   kinatokana na  Ustawi wa Uhuru wa  wananchi. Nafasi pana ya ukosoaji  , utoaji maoni , ushauri huku wakipata maelezo toka Serikalini .

Alisema ni nchi chache sana  duniani zenye kufuata  Mfumo wa demokrasia   inayolingana na  utaratibu uliopo Tanzania. 

 " Abadan sina shaka na aina ya demokrasia yetu Tanzania .Tuna ustawi mkubwa wa  demokrasia  iliovuka mipaka. Leo kuna wanaofika hadi kutukana viongozi bila sababu hawakatwi  .Ni  demokrasia yenye rutuba,  kinga na Uvumilivu"  Alisema Mbeto 


Katibu huyo Mwenezi  alisema ni nadra kuikuta aina ya demokrasia hiyo katika Mataifa mengine kama ilivyo  Tanzania,  lakini  yote hiyo imetokana na  dhima ya Ukomavu wa kisiasa  ,Uvumilivu ,Ujenzi mpya wa Taifa ,Mapatano na Maridhiano 

Akijibu swali kuhusu msimamo wa chama chake wa   kuandika katiba mpya, Mbeto  alisema kabla Rais Dk Samia Suluhu Hassan hajamaliza muda wake madarakani kikatiba , serikali yake itawapatia Waatanzania Katiba Mpya.

"Wakati Dk Samia alipokuwa akizindua kampeni ya Uchaguzi Mkuu wa  chama chetu  katika Viwanja vya Tanganyika Peckers,  amewaahidi  Watanzamia Serikali yake itawapatia Katiba mpya" Alisema

Kadhalika Mbeto  alisema ajenda ya Katiba mpya  ni ya Serikali  za CCM,  si ya  upinzani ,  Tume zote za Ukusanyaji Maaoni ya Wananchi  zimeundwa  na Serikali zilizo madarakani. 

"Itaandikwa  Katiba mpya itakayozingatia ushauri na maoni yote ya Wananchi. Itapitia  na kuzingatia mapendekezo ya Tume   za  Jaji   Nyalalai, Jaji Kisanga, Jaji  Warioba na Jaji  Chande"   Alisistiza 

Hata hivyo , Mwenezi  huyo alisema  Katiba Mpya   itafuata   Ushauri  uliotolewa na wananchi,kulinda tunu za taifa , ustawi wa Kisiasa ,uboreshaji mifumo ya Uchaguzi na kuwashrikisha  wadau wa maendeleo ya  domokrasia.

Post a Comment

0 Comments