Na Victor Masangu,Pwani
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Pwani katika kipindi cha miaka kumi iliyopita kuanzia mnamo mwaka 2015 hadi mwaka 2026 imefanikiwa kufanya vizuri baada ya kukusanya kodi kiasi cha shilingi bilioni 266.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa TRA Mkoa wa Pwani Peter Eliona wakati wa halfa ya kongamano maalumu ambalo limewajumuisha wadau mbali mbali pamoja na walipa kodi ikiwa ni katika kuelekea maadhimisho ya miaka 30 ya TRA.
Meneja huyo amebainisha kwamba fedha hizo zimekusanywa kutokana na kuwepo kwa mfumo mizuri waliyoiweka katika suala zima la ukusanyaji ikiwemo pamoja na kuwashirikisha walipa kodi.
Aidha meneja huyoo amesema kwamba lengo kubwa TRA ni kuendelea kuweka mikakati ya kuendelea kukusanya kodi ambayo imekuwa ni mkombozi katika kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo.
"Leo tumekutana katika kongamano hili ambalo tumeweza kuwashirikisha sadau wetu wa maendeleo pamoja na walipa kodi ili kuweza kujadili mambo mbali mbali ya ulipaji wa kodi,"amebainisha Meneja huyo.
Naye Mwenywkiti wa Chama cha Wafanyabiashara Mkoa wa Pwani Abdallah Ndauka amesema ili kuongeza makusanyo TRA wanatakiwa kuangalia namna ya kuwasaidia wafanyabiashara wasifunge biashara zao badala yake wajikite kushauri kuwasaidia kuendelea zaidi.
Amesema kwamba wapo wafanyabiashara wanafunga biashara zao kutokana na sababu mbalimbali ili kunusuru hilo ni vema watumishi wa Mamlaka hiyo wakawa msaada wa kuzifufua ili waendelee kupata kodi.
Pia, ameiomba TRA mkoa wa Pwani kuwa sehemu ya kutoa fursa kwa wafanyabiashara hao ili kukuza biashara zao kwa kununua vifaa na samani nyingine badala ya kuagiza nje ya nchi.
Mamlaka ya Mapato (TRA)) Mkoa wa Pwani imekuwa ikishirikiana bega kwa bega na walipa kodi pamoja na kutoa mafunzo ambayo yamesaidia kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato na kuvuka malengo.

0 Comments