NCAA YAWAPIGA MSASA MALAIGWANAN







NA MWANDISHI WETU

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imeendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa Malaigwanani ,wazee na kina mama maarufu wapatao 33 kutoka kata 11  za ndani ya eneo la hifadhi Ngorongoro ili kuwajengea uwezo wa kutambua fursa mpya za kiuchumi.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Kamishina Msaidizi  Mwandamizi anayeshughulikia huduma za jamii bi  Gloria Bideberi amesema lengo la semina hiyo ni kuhakikisha Malaigwanani na wazee hao wanapata elimu ya kutosha kuhusu ujasiriamali na namna ya kutumia fursa zinazopatikana katika maeneo yao.

Bi. Gloria alieleza  kwamba elimu hiyo itakwenda  sambamba na ziara za kujifunza kwa vitendo, ambapo washiriki watatembelea maeneo mbalimbali ya uzalishaji wa bidhaa ikiwemo kiwanda cha uzalishaji wa bidhaa za maziwa Tanga Fresh kilichopo Mkoani Tanga ili kujifunza namna bidhaa zinavyozalishwa, kuendelezwa na kufikishwa katika masoko.

“Lengo la mafunzo haya ni  kuhakikisha kuwa wananchi hawa wanapata elimu ya kutosha na kuwawezesha kutembelea maeneo mbalimbali ya uzalishaji wa bidhaa ili kujifunza kwa vitendo zaidi,” alisema Gloria 

Mafunzo hayo ni sehemu ya juhudi za Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro katika kuwawezesha wananchi kiuchumi na kuimarisha ushiriki wa jamii katika maendeleo endelevu ya eneo la Hifadhi Ngorongoro.

Post a Comment

0 Comments