WILAYA YA NGORONGORO KUZALIWA UPYA



NA MWANDISHI WETU

Wilaya ya Ngorongoro ipo katika hatua za mwisho ya mapitio na kupitisha mkakati mpya wa miaka mitano unaodhamiria kufanya mageuzi makubwa ya kiuchumi, kijamii na kasi ya maendeleo unaokwenda sambamba dira ya taifa ya maendeleo 2025-2050.

Akifungua kikao maalum cha kupitia mkakati huo  mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Brigedia Jenerali Wilson  Sakulo amewataka madiwani wa halmashauri hiyo kutumia fursa hiyo kwa kupanga vipaumbele vitakavyogusa maisha ya wananchi.

“Leo tumekutana hapa kupanga mipango yetu  kwa miaka mitano, hakikisheni mnapanga  vipaumbele vinavyopimika kwa kuangalia maslahi ya wananchi wa wilaya hii ili waweze kupata huduma bora za kijamii, miundombinu na kuboresha shughuli zao za kiuchumi”,alisema Brigedia Jenerali Sakulo.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro Mhe. Manja Sironga Yaile aliipongeza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kuendelea kuwa mdau muhimu wa maendeleo kutokana na kushiriki kikamilifu katika kuchangia mipango mbalimbali ya kijamii ya Tarafa ya Ngorongoro na wilaya hiyo.

Wakichangia kuhusu mpango mkakati huo baadhi ya madiwani walisisitiza umuhimu wa kujikita katika ujenzi wa barabara,malisho, maji na uimarishwaji wa huduma za kijamii.

Post a Comment

0 Comments