Mbeto asema Dk Mwinyi yuko ughaibuni akiwinda fursa za Uwekezaji



Na Mwandishi  Wetu, Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi kimesema Rais wa Zanzibar  Dkt. Hussein Ali Mwinyi yuko nchini Qatar  katika mawindo ya kushiriki fursa  za  kiuchumi na uwekezaji kwa ajili ya maendeleo ya Zanzibar 

CCM kimeitaja  ziara hiyo  ya kikazi  pia ina madhumuni  ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kiuchumi kati ya Zanzibar na Qatar.

Hayo yametamkwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar ,Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis,  aliyeitaja ziara hiyo  ni muhimu kwa maendeleo ya Zanzibar. 

Mbeto alisema pamoja na ziara hiyo kuwa   sehemu ya juhudi za  SMZ kujenga uchumi  imara  ,itaimarisha diplomasia ya kiuchumi, kuvutia uwekezaji na kukuza ushirikiano wa kimkakati kwaajili ya msukumo wa maendeleo. 

Alisema zama hizi maendeleo ya Kijigitali, Sayansi na Teknolojia , si zama za Rais  wa nchi kujifungia  ikulu, bali ni nyakati za kutoka ,  kuhemea mawindo na  na kunasa fursa  za uwekezaji .

"Ziara ya Dk mwinyi huko Doha nchini Qatar ni ya  mawindo ya fursa za  kiuchumi. Dunia ya leo imekuwa  kijiji kidogo .Lazima utoke kwa ajili  ya kushiriki mijadala inayohusu fursa na kuimarisha uhusiano"Alisema Mbeto 

Aidha akiwa  nchini humo,Rais Dk Mwinyi atatembelea kuona huduma za Afya katika kituo cha DOC Medical Center nchini Qatar ambacho ni kituo cha huduma za Afya kinachotoa huduma zake kupitia idara nane za kitaalamu katika sekta ya Afya.

Katika ziara hiyo, Rais Dkt. Mwinyi  atashuhudia uendeshaji wa masuala kadhaa  katika sekta ya Afya kupitia Wizara ya Afya ya nchi hiyo.

"Chama chetu kimempa baraka na mkono wa pongezi Rais  Dk Mwinyi kwa juhudi za kuifanyia mageuzi  Zanzibar. Unapohangaikia mawindo ya kujenga uchumi na uwekezaji lazima tuimarishe sekta ya Afya  "Alieleza.

Katibu  huyo Mwenezi  amewahakikishia wananchi kuwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilio chini ya umoja wa kitaifa, itafanya kila linalowezekana kuhakikisha Zanzibar inasongambele kimaendeleo.

Post a Comment

0 Comments