Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Chama Cha Mapinduzi kimewataka wanachama wake kujua kuwa umoja,mshikamano na ushirikiano ndani ya chama ,ndio msingi wa ushindi kwa chama hicho.
Pia chama hicho kimeapa kutomvumilia Mwanachama wake yoyote atakaebainika kuunda makundi ya mgawanyiko.
Hayo yametamkwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo,Khamis Mbeto Khamis na kusema chama cha siasa maakini siku zote kinahitaji umoja, upendo na ushirikiano .
Mbeto alisema kila Mwanachama au Kiongozi wa CCM , anapaswa kujua lengo kuu la chama hicho ni kushinda chaguzi zote za dola, hivyo umoja na ushirikiano ni kipaumbele namba moja.
Alisema Uchaguzi ndani ya chama unapomalizika , Wanachama hutakiwa kuwa wamoja , na yeyote atakaebainika anaendeleza makundi , ataadhibiwa kwa mujibu wa katiba na kanuni za chama .
"Umoja na Mshikamano huchochea kuni za ushindi . Asitokee wa kutugawa au kudhoofisha malengo yetu .Tutaendelea kushinda na kushika dola kwa ridhaa ya wananchi " Alisema Mbeto.
Aidha, Katibu huyo Mwenezi aliwataka viongozi wa chama katika ngazi zote, kufanyakazi za chama ndani ya chama,nje na ndani ya umma kwa umakini na bidii.
Katibu huyo Mwenezi alieleza kuwa ,CCM kitaendelea kuhimiza Umoja, ushirikiano na Mshikamano, kama nyenzo kuu za kukipatia chama ushindi wa kishindo

0 Comments