MBETO: HAKUNA SERIKALI DUNIANI INAYOWATAKIA MABAYA WANANCHI WAKE


Na Mwandishi Wetu ,  Zanzibar

Chama Cha Mapinduzi kimeitaka  Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar (SMZ) kuendelea kusimamia  mpango  mkakati wake wa kuwataka wakaazi  katika  eneo la  Kiilimani Kisiwani Unguja kuhama ili kupisha ujenzi mpya. 

Kadhalka  CCM kimewashauri   Wakaazi wote  wanaoishi kwenye Maghorofa hayo , kukubaliana na uamuzi wa SMZ,  unaowataka kupisha Ujenzi wa Mradi wa  Nyumba za kisasa. 

Rai hiyo  imetolewa na Katibu wa Kamati  Maalum  ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis aliyesema hakuna Serikali inayowaombea wananchi wake wakumbwe na  majanga .

Mbeto alisema kwa muda mrefu SMZ  imekuwa akiwashauri   Wakaazi wa eneo  la Kilimani  ambalo lipo   karibu na ufukwe wa Bahari, kuhama ili kuupisha  ujenzi wa Mradi wa Mji mpya .

Alisema Serikali  ya Awamu  ya Nane chini ya Rais  Dk Hussein Ali Mwinyi , ilipeendekeza  mpango madhubuti uitwao  Dk Mwinyi Smart City , lakini ghafla  yakazuka  mabishano yenye upotoshaji uliovunja dhamira njema . 

"Hakuna Serikali yoyote duniani inayowatakia maafa au  mabaya  Wananchi wake .Eneo  la Ardhi   la Kilimani linakabiliwa na   Mmong'onyoko mkali wa Ardhi . Hakuna njia mbadala zaidi ya kubomoa Nyumba Kongwe na  kujenga majengo mapya ya kisasa " Alisema Mbeto .

Aidha, Katibu  huyo Mwenezi  ,alisema  licha ya juhudi za awali za SMZ , kuwataka  Wakaazi wa eneo hilo  kuhama kwa hiari  , waligoma kwa kusikiliza maneno yenye kuwavunja nguvu na  ushabiki   wa kisiasa. 

"Tumepokea taarifa za  kuporomoka kwa baadhi ya Nyumba za Kilimani . Nyumba zile zilikuwa kongwe na si salama kwa  Makaazi
ya binadamu   .Tunaielekeza SMZ  iendeleee na mkakati wake wa   kujenga Mji mpya  wa kisasa "Alieleza.

Mbeto aliwataka wakaazi wa maeneo  hayo kuutafakari   ule usemi wa Kiswahili,  usemao  akili za kuambiwa changanyag na zako, hivyo ni lazima wakaazi hao watii na kukubaliana na  mpango wa Serikali wa Ujenzi mpya. 

"Tutaishangaza dunia  ikiwa Wananchi Wakazi wa maeno hayo wataendelea kukaidi  na kutaka   kuishi katika majengo   hatarishi. Serikali isikubali  kusubiri hadi maafa yatokee. "Alisisitiza.

Mbeto  alisema mara baada ya Ujenzi  huo kukamilika chini ya  viwango bora ,  salama na madhubuti,  wananachi waliokuwa na nyumba zao ,watapewa nyumba mpya huku Serikali chini ya mradi huo  ikipangisha nyumba zake .

'Tuiamini nia njema alionayo Rais  Dk Mwinyi na Serikali yake. Ushindani wa Kisiasa usiingilie na kutaka kuvuruga Usalama wa  maisha ya watu. Nia na Sera za CCM ni kuiona Zanzibar ikisongambele "Alisema Mbeto

Post a Comment

0 Comments