Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete (kulia) akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa naSerikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa wakati wa uzinduzi wa operesheni maalum ya kukamilisha uwekaji anuani za makazi nchini uliofanyika ukumbi wa mkutano wa Jakaya Kikwete Convention Centre Dodoma jana.
NA MUNIR SHEMWETA, WANMM DODOMA
WIZARA
ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imekamilisha uandaaji ramani za
kidijitali zinatotumika kama ramani za msingi kwenye utekelezaji mfumo wa
anuani za makazi katika halmashauri 38 nchini.
Aidha,
Wataalamu wa Wizara ya Ardhi wanaendelea kutekeleza kazi ya kubadilisha ramani
kutoka kwenye mfumo analogia kwenda digitali na kutambua maeneo yasiyo pimwa,
kuandaa ramani za mipaka ya kiuatawala katika halmashauri mbalimbali nchini.
Hayo
yalibainishwa jana na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Ridhiwani Kikwete wakati wa uzinduzi wa operesheni maalum ya kukamilisha
uwekaji anuani za makazi nchini uliofanyika ukumbi wa mkutano wa Jakaya Kikwete
Convention Centre Dodoma.
Kwa
mujibu wa Ridhiwani, Wizara ya Ardhi imejipanga kikamilifu kuhakikisha zoezi za
uandaaji ramani za kidigitali linakamilika ndani ya muda ili kuwezesha utoaji
anauani za makazi.
‘’Wizara
tutanufaika sana na taarifa zinazokusanywa kwenye mfumo wa anuani za makazi
kutokana na kutumia taarifa hizo kuhakikisha tunaboresha taarifa zilizopo
kwenye mifumo ya usimamizi wa ardhi, kuimarisha ukusanyaji mapato ya ardhi
pamoja na kuboresha utoaji huduma za ardhi kwa kutumia anuani za makazi.
Naibu
Waziri wa Ardhi aliongeza kwa kusema, zoezi hilo la kubadilisha ramani kutoka
mfumo wa analogia kwenda digitali lilianza katika halmashauri zote tano za mkoa
wa Dar es salaama, jiji la Dodoma pamoja na halmashauri nyingine za mikoa ya
Tabora, Kagera, Tanga na Mbeya.
‘’Iwapo
zoezi hili likifanyika kikamilifu nchi nzima litawezesha Wizara ya Ardhi
kuongeza uwezo wa kusimammia uendelezaji miji, utatuzi wa migogoro ya ardhi kwa
njia ya kidigitali kwa kuwa ramani zote za mipango miji na upimaji nchini
zitakuwa kwenye mfumo huo zikibainisha viwanja au mashamba matumizi
yake’’. Alisema Ridhiwani
Alisema,
ulinganifu wa kitakwimu utawezesha Wizara ya Ardhi kutoa huduma bora zaidi na
kusimamia upatikanaji taarifa za wamiliki wa ardhi kupitia mfumo unganishi wa
taarifa za ardhi ILMIS. Pia utarahisisha kutambua maeneo kwa ajili ya
uwekezaji, na shughuli mbalimbali kama makazi mashamba na maeneo ya kufugia na
shughuli za uchumi.
Hata
hivyo, mbali na faida za kitakwimu zinazopatikana kwenye zoezi la anuani za
makazi alibainisha kuwa, lengo la uandaaji ramani hizo ni kurahisisha
upatikanaji taarifa sahihi za ardhi ambazo ni muhimu katika kujenga msingi wa
anuani za makazi pamoja na utekelezaji maono ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha ardhi inapangwa, napimwa na
kurasimishwa.
0 Comments