Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam ACP Muliro Jumanne Muliro.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Dar-es-salaam 16/06/2022
JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM LIMEWAKAMATA WATUHUMIWA 396 KWA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA VITENDO VYA KIHALIFU
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Vyombo mbalimbali vya Dola na Raia wema linaendelea na Operesheni kali maalum iliyoanza tarehe 15/05/2022 hadi 15/06/2022 katika maeneo mbalimali ya Jiji la Dar es salaam,Lengo ni kuzuia na kukabiliana na vitendo vya kihalifu kama Unyang’anyi wa kutumia silaha, Wizi wa magari na vipuli, Wizi wa pikipiki, Uvunjaji, madawa ya kulevya na vitendo vya ukatili wa Jinsia.
Unyang’anyi wa kutumia silaha.
Watuhumiwa Mohamed Bakari Mremi na wenzake 12 walikamatwa kwa tuhuma za kupanga, kujihusisha na kutekeleza matukio mbalimbali yaliwemo ya kutumia silaha kama mapanga, nondo , visu na pia kupitia falsafa ya ulinzi shirikishi zilipatikana bastola mbili moja aina ya TAURUS silver namba P-22 cariba FL CAR- 22 LR iliyotengenezwa Miami nchini Marekani ikiwa na risasi mbili na ya pili aina ya BROWNING IKIWA NA RISASI 42.
Uvunjaji , Watuhumiwa Omary Bwilani, miaka 34, mkazi wa Buza na wenzake 54 walikamatwa wakiwa na Tv 08 za wizi zenye ukubwa tofauti, sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania pair 3, buti pair 1, kofia 1, DVD player 1 na fedha taslim Tshs. 300,000/=zilizoibwa , Hatua za kisheria zitafuatwa kuwafikisha wahusika kwenye vyombo vya kisheria.
Baadhi ya Wezi wa magari na vipuli vya magari, Watuhumiwa 15 wamekamatwa -
01.Magari mawili moja lenye namba za usajili T.617 DRU aina ya Suzuki Carry na la pili aina ya Toyota Wish nyeusi ambalo limefutwa namba za usajili na kubadilishwa rangi kuwa rangi nyeupe.
02. Side mirrors za magari mbalimbali - 38
03. Plate numbers za magari mbalimbali - 47
04. Gear box moja ya gari aina ya Toyota Hilux
05. Taa za nyuma za magari mbalimbali- 14
06 Taa za mbele za magari mbalimbali- 21
07. Engine tatu za pikipiki
08. Exhost pipe moja ya gari
09. Rim sita size 15 za magari madogo
10. Mlango mmoja wa abiria wa gari aina ya Toyota Prado
11. Leseni moja ya biashara inayodhaniwa kuwa ya kughushi
12. Kadi za usajili wa magari mbalimbali zipatazo- 26
13. Mkataba wa uongo wa mauziano ya gari.
Watuhumiwa wanahojiwa kwa kina ili watuoneshe yalipo magari ya no tulizowakuta nazo na mifumo ya kisheria itafuatwa katika kushughulika na kundi hili
Wizi wa piki piki
Ufuatiliaji ulifanywa maeneo ya Kigamboni, Mbagala, Tegeta, Kunduchi, Tabata, Gongo la Mboto na Chanika, ambapo walikamatwa Thabit Idd, miaka 28, mkazi wa Gezaulole na wenzake 24 wakiwa na Pikipiki 15 pamoja na Fedha Taslim Tshs. 2,600,000/= ambazo ni zao la biashara isiyohalali ya wizi wa pikipiki. Watuhumiwa wataendelea kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria
Madawa ya kulevya na Pombe haramu ya Moshi
Katika eneo hili Watuhumiwa 206 walikamatwa wakiwa na madawa aina mbalimbali ya kulevya ikiwemo Heroine Gm 93, Bhangi Kg 222 na Gm 109, na mirungi kg 3.5 Watuhumiwa wamefikishwa Mahakamani.
Sambamba na hilo Watuhumiwa 81 akiwemo Fatuma Juma, miaka 43 mkazi wa Tundwi Kigamboni na wenzake 80 walikamatwa kwa tuhuma za kupatikana na Pombe moshi lita 124 na mitambo 06 ya kutengeneza Gongo. Watuhumiwa walihojiwa na kufikishwa
Mahakamani.
UKATILI WA KIJINSIA
Kesi kadhaa zimetolewa taarifa kwenye vituo vya Polisi mkazo maalum umewekwa ili kesi hizi zipelelezwe haraka na baadhi ya
Watuhumiwa wamefikishwa Mahakamani akiwemo Joshua Simangwe, miaka 66, mkazi wa Kipunguni Ukonga anayetuhumiwa kuwalawiti watoto watatu wenye umri chini ya miaka 18 ambao ni wanafunzi huko maeneo ya Gongolamboto Dar es salaam.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linamtafuta Godbles Sawe, miaka 47, Mchaga, fundi Friji mkazi wa Kimara Suka kwa tuhuma za kumuua mke wake Ester Benito Gadau kwa kumkata kwa kitu chenye ncha kali kichwani tarehe 14/06/2022 huko maeneo ya Kibamba Wilaya ya Ubungo na kukimbia baada ya kutekeleza mauaji hayo.
Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam linamshikilia FRANK PATRICK BARNABAS ambaye amekuwa akijifanya Askari Polisi huku akifanya uhalifu wa kutapeli watu na kupita kwa watu mbalimbali madukani kuwa anatafuta vipuri vya gari la Polisi huku akishirikiana na tapeli JOHN JOSEPH SHIJA anayejifanya fundi wa gari za Polisi. Watu hawa si askari, Taratibu za kisheria zinakamilishwa ili wafikishwe mahakamani.
Jeshi la Polisi linaendelea kuwashukuru wananchi wanaoshiriki moja kwa moja katika ulinzi shirikishi, kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu. na kuiishi falfasa ya Polisi jamii
Muliro J. MULIRO– ACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM DAR Es SALAM.
0 Comments