MAFUNZO MAALUM YATOLEWE KABLA YA MIKOPO YA ASILIMIA 4 KUTOLEWA



Na Mwandishi Wetu, Lewa/Bungu Korogwe 

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mary Chatanda (MCC ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Vijiji Mkoani Tanga kutoa Mafunzo kwa makundi ya akina mama, vijana na watu wenye ulemavu kabla ya kupewa mikopo ya asilimia kumi Ili kuwaletea maendeleo pamoja na kuirejesha kwa wakati.

 "Mafunzo maalum yanayohusu usimamizi wa fedha na miradi yanapaswa kutolewa ili  kuwawezesha wanufaika wa mikopo ya asilimia nne (4) hususani akina mama kuweza kutumia mikopo hiyo vizuri pamoja na kuirejesha kwa wakati na kutoa fursa kwa wengine kuweza kukopeshwa mikopo hiyo" amesema Chatanda.

Chatanda ameyasema hayo hii leo Ijumaa Oktoba 18, 2024 wakati wa zoezi lake la Kuhamasisha  Wananchi kwenda Kujiandikisha katika Kata ya Lewa, Lutindi na Bungu Wilayani Korogwe.

Post a Comment

0 Comments