Na Victor Masangu,Kibaha
Diwani wa kata ya Pangani Mhe. John Katele ameahidi kuchangia mifuko 10 ya simenti kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa chuo ambacho kitakuwa kinatumika kama madrasa kinachotarajiwa kujengwa katika eneo la mtaa wa vikawe Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Mkoa wa Pwani.
Mhe. Katele ametoa ahadi hiyo wakati wa halfa fupi iliyoandaliwa maalumu kwa ajili ya kufanya mchango wa harambee kutoka kwa viongozi na wadau mbali mbali kwa lengo la kuweza kusaidia katika suala zima la kuwezesha ujenzi wa chuo hicho cha madrasa kwa watoto.
"Nashukuru nimeweza kualikwa katika halfa hii fupi nikiwa kama diwani wa kata ya Pangani na lengo langu kubwa ni kuendelea kushirikiana bega kwa bega na wananchi wangu katika mambo mbali mbali ya kijamii hususan jambo hili la ujenzi wa chuo cha madrasa na mimi nitachangia mifuko kumi ya simenti,"amebainisha Diwani Katele.
Aidha Diwani huyo amewahimiza watoto hao ambao watakuwa wanakitumia chuo hicho madrasa pindi kitakapokuja kukamailika kuweka misingi imara ya kuwa na upendo na mshikamano wa pamoja ambao utaweza kuwasaidia kufika mbali katika kujifunza mambo mbali mbali yananayohusu masuala ya dini.
Katika hatua nyingine amewaomba wadau mbali mbali na viongozi sambamba na wananchi kujitolea kwa hali na mali katika kuchangia michango mbali mbali ambayo itaweza kusaidia kukamilika kwa chuo hicho cha madrasa ambacho kinatarajiwa kujengwa katika Kata ya Pangani.
.jpeg)

0 Comments