IGP WAMBURA AWASISITIZA WAHITIMU WA KOZI ZA TAALUMA YA POLISI KWENDA KUTOA HUDUMA BORA KWA JAMII.


 DAR ES SALAAM

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP, Camillus Wambura,  amewakumbusha Askari wa vyeo mbalimbali,ikiwemo Wakaguzi na Maafisa wa Jeshi hilo kuwa, jukumu lao kubwa na la msingi ni kuwahudumia wananchi,

Aidha,IGP wambura amesema ili huduma ziwe bora ni lazima Jeshi la Polisi lifanye tathmini ya mara kwa mara kwa lengo la kubaini ikiwa ujuzi na maarifa (weledi) wa watendaji wake unakwenda sambamba na matarajio ya wanan chi, pamoja mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

IGP Wambura ameyasema hayo leo mapema Jijini Dar es Salaa wakati akiwatunuku wahitimu 559 wa kozi mbalimbali za Kitaaluma ikiwemo Astashahada na Stashahada zinazotolewa na Vyuo vya Taaluma ya Polisi nchini vinavyotoa Taaluma ya Sayansi ya Polisi, Taaluma ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Taaluma ya Stadi za Mawasiliano ya Polisi na Taaluma ya Usalama Majini.

IGP Wambura amesema kuwa, suala la kujiendeleza kielimu na umuhimu wake  linachagizwa na maneno ya hekima kutoka Mithali 4:13 yasemayo 'Mkamate sana elimu, usimuache aende zake; mshike maana yeye ni uzima wako.

Sherehe za Mahafali hayo ya 9 ya Vyuo vya Taaluma ya Polisi Tanzania zimefanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa serikali, wananchi pamoja na askari wav yeo mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments