MABATI ZONE TANZANIA YAIMWAGIA VIFAA VYA MICHEZO TIMU YA BUGURANI VETERANI





Mkurugenzi Mtendaji wa Mabati Zone Tanzania Mikidadi Athumani (katikati) na wawakilishi wa Timu ya Buguruni Veterani wakionesha jezi watakazotumia kwenye Ligi ya Maveterani inayotarajia kuanza hivi karibuni.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mabati Zone Tanzania Mikidadi Athumani akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Wakati wa kuikabidhi vifaa vya michezo timu ya Buguruni Veterani.


Hizo ni miongoni mwa bidhaa za mabati zinazopatikana Mabati Zone Tanzania.

NA MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya Mabati Zone Tanzania imeikabidhi Timu ya Buguruni Veterani vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 3.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 24, 2025 jijini Dar es Salaam katika hafla ya makabidhiano hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Mabati Zone Tanzania Mikidadi Athumani amesema vifaa hivyo Timu ya Buguruni Veterani itavitumia kwenye Ligi ya Maveterani inayotarajia kuanza hivi karibuni.

Athumani amevitaja vifaa hivyo kuwa ni pamoja na Jezi za Timu hiyo za Nyumbani na Ugenini, za magoli kipa na za makocha, lakini pia amewakabidhi mipira ambayo wataitumia kwa ajili ya Maandalizi ya Ligi hiyo ambayo miongoni mwa Timu zitakazoshiriki ni Timu za Maveterani wa Simba na Yanga.

"Lengo la kukabidhi vifaa hivi vya michezo kwa Timu ya Buguruni Veterani ni kwa ajili ya ushiriki wao wa Ligi ya Maveterani. Licha ya Mimi mwenyewe kuwa CEO wa Mabati Zote Tanzania, lakini pia ni mchezaji," amesema Athumani na kuongeza,

"Hivyo tunataka vifaa hivi viwe kichocheo kwa Timu yetu kufanya vizuri kwenye Ligi hii, na ninaamini itafanya vizuri kwa sababu ina wachezaji wazuri na wanaendelea kujiandaa vizuri ili kuzidi  kujiimarisha kwa ajili ya ushindani,".

Hata hivyo amesema kuwa kupitia udhamini wa vifaa hivyo kwa Timu hiyo utaifanya Kampuni ya Mabati Zone Tanzania kutambulika kwa Watanzania wote, lakini pia kuweza "kusapoti" wengine wanaohitaji "sapoti" yao.

Mkurugenzi huyo ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wanamichezo wengine kushiriki katika masuala ya michezo.

Katika hatua nyingine akizungumzia kuhusu badhaa za Mabati ambazo zinapatikana katika Kampuni hiyo ya Mabati Zone Tanzania amewakaribisha Watanzania kuhakikisha wanajenga kwa kutumia Mabati hayo kwani ni Imara na Bora ambayo yanadumu kwa muda mrefu bila kupoteza ubira wake.

Ameeleza kuwa mteja anayenunua kwao Mabati anasafirishiwa bure hadi nyumbani kwake hata kama ni mteja wa mkoani 

"Tuna Mabati ya aina mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Mabati ya migongo mipana, Kampuni yetu ni kubwa na tunakushauri kuezeka kwa mabati Bora kutoka Mabati Zone Tanzania," ameongeza Athumani.

Amesema kuwa wamekuwa wakitoa elimu ya Mabati, lengo likiwa ni Watanzania waweze kutambua aina mbalimbali za mapati zinazopatikana kwa ajili ya uezekaji wa Mabati Bora.

Kwa upande wake Kocha wa Timu ya Buguruni Veterani Omary Mbweze ameishukuru Mabati Zone Tanzania kwa kuwakabidhi vifaa hivyo kwa ajili ya Ligi ya Maveterani.

Ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wadau wengine kujitokeza na kuwaunga mkono Buguruni Veterani.

Kuelekea Ligi hiyo, Kocha huyo ameeleza kuwa anamatumaini watafanya vizuri kwani wamefanya usajili mzuri, hivyo ametoa wito kwa wakazi wa Buguruni kuwaunga mkono kwa kujitokeza kuwashangilia siku wanayocheza.

Mawasiliano Mabati Zone Tanzania: 0766 616 676

Post a Comment

0 Comments