MADIWANI KIBAHA TC WATOA MATAMKO YA KUMPONGEZA RAIS DKT.SAMIA




NA  VICTOR MASANGU, KIBAHA
 
Baraza la madiwani katika  Halmashauri ya Kibaha mji  limetoa tamko na kuazimia  rasmi  kwa pamoja  kumpongeza Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuridhia maombi na kuweza kuipandisha adhi Halmashauri hiyo kuwa Manispaa pamoja kuteuliwa  na mkutano mkuu  maalumu  kuwa mgombea wa nafasi ya Urais pamoja na mgombea mwenza  Dkt. Emmanuel Nchimbi.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibaha mji Mussa Ndomba  katika kikao cha baraza la madiwani la kawaida kwa kipindi cha robo ya pili ambapo amesema kwamba wameamua kwa kauli moja wanampongeza kwa dhati kupitishwa kwa kishindo na wajumbe wa mkutano huo.
 
Aidha Ndomba amebainisha kwamba baraza hilo limepongeza Rais kwa kutenga fedha nyingi  ambazo zimeweza kuleta chachu  kubwa katika suala zima na utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo katika sekta ya elimu, afya,  maji pamoja na miundombinu ya barabara ya maendeleo.

"Kwa kauli moja baraza la madiwani tunatoa pongezi kubwa kwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuipandisha adhi Halmashauri yetu ya mji Kibaha kuwa manispaa, pamoja kuteuliwa kuwa mgombea wa nafasi ya Urais ikiwa sambamaba na mgombe mwenza Dkt. Emmanuel Nchimbi kupitia chama cha mapinduzi (CCM) katika uchaguzi wa mwaka 2025.

Pia katika hatua nyingine baraza hilo la madiwani limemuomba Rais kuwapatia eneo la shirika la elimu Kibaha kwa ajili ya kuweza kuliendeleza ikiwa sambamba na  kupanga mji katika mambo mbali mballi ya huduma za kijamii sambamba na kurudisha huduma ya mabasi ya mwendo kasi kama ilivyokuwa hapo awali  kwani kwa sasa wananchi wanapata shida sana.  

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson John amaipongeza Halmashauri ya mji wa Kibaha kwa kuweza kupandishwa adhi kuwa Manispaa pamoja na kuweka juhudi katika suala zima la ukusanyaji wa mapato.

Aidha amesema kwamba Halmashauri ya Kibaha mji kwa sasa inabidi kubadilika na kuhakikisha kwamba wanaweka mikakati ya kupima viwanja ambavyo ni mashaba pori na kuweka mipango ya  kuweza kuwapatia hati ndani ya wiki moja.

                           MWISHO

Post a Comment

0 Comments