NA MWANDISHI WETU
MSANII wa Muziki wa Kizazi Kipya Clayton Chipando Maarufu kama Baba Levo, amesema kwa kushirikiana na Online Media watazunguka mikoa 15 nchini kuangazia utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi chini ya uongozi wa Mwenyekiti Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kipindi cha miaka minne cha utawala wake.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 3, 2025 jijini Dar es Salaam Baba Levo amesema wataanza na mikoa nane ambayo ni Mwanza, Kigoma, Arusha, Dodoma, Geita, Katavi, Kilimanjaro na Dar es Salaam.
"Tunataka Online Tv zote Tanzania, kwa pamoja tukaangazie yaliyofanywa na Chama cha Mapinduzi chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan," amesema Baba Levo.
Baba Levo amesema kuwa wataanda na kueleza "MAMA HANA DENI" Kwa maeneo yote ambayo Ilani ya CCM imetekelezwa Kwa utekelezaji wa Mradi ya Maendeleo.
"Tukaonyeshe kwamba "MAMA HANA DENI", lengo ni kwenda kuangazia miradi yote iliyotekelezwa na Rais Samia. Tukamsapoti Rais kwa kutekeleza Ilani ya CCM ya 2020-2025, aliyotenda mema tutayasifia. Na yale ambayo bado yanahitaji utekelezaji kwa kuongeza nguvu tutayasema," amesisitiza Baba Levo.
Ametaja baadhi ya miradi ambayo imetekelezwa kuwa ni ujenzi wa Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere, Uj nzi wa Nyumba za Kisasa katika Mji wa Dodoma, ukamilishwari wa Reli ya Kisasa ya SGR na kuanza Kwa safari za treni ya mwendokasi Kwa Dar es Salaam hadi Dodoma.
Katika hatua nyingine Baba Levo amesema kuwa wanatarajia kuanzisha Umoja wa Online Tv kwamba Online tv kwa sasa zimekuwa nyingi na kila mtu anafanya kwa namna yake.
Hivyo amesema watu wa Online Tv wanapaswa kuwa na umoja wao, na wawe na mahali pakusemea ambapo hata mmoja wao akitokewa na tataizo wanaweza kumsaidia.

0 Comments