KAMISHNA WA UHIFADHI TANAPA, CPA KUJI AONGOZA KIKAO KAZI CHA MENEJIMENTI YA SHIRIKA




NA MWANDISHI WETU

Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, CPA Musa Nassoro Kuji leo Desemba 02, 2025 ameongoza kikao kazi cha Menejimenti ya Shirika kilicholenga kupokea taarifa ya mapitio ya tathmini ya marejeo ya mpango mkakati wa Shirika wa mwaka 2021/2022 - 2025/2026 ili kutumia uzoefu uliopatikana wakati wa utekelezaji kuandaa Mpango Mkakati mpya wa Shirika wa mwaka 2026/2027 hadi 2030/2031. 

Mpango Mkakati wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) unazingatia ushirikishwaji mpana na ulinganifu wa vipaumbele vya Taifa kama vile Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP IV), Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050, Ilani ya Chama Tawala pamoja na Mikataba ya Uhifadhi ya Kikanda na Kimataifa.

Kikao hicho pia kilihusisha wawezeshaji kama vile Mkurugenzi wa Tathmini na Ufuatiliaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bi. Sakina Mwinyimkuu, Mshauri Elekezi kutoka Chuo Kikuu Dodoma Dkt. Wilhelm Kiwango na Afisa Uhifadhi Mkuu Herbet Lyimo wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Ulemavu.

Post a Comment

0 Comments