Na Mwandishi Maalum, Pemba
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimeridhishwa na zoezi la Uandikishaji kwenye Daftari la Mpiga kura katika Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba kwa mujibu wa sheria na kwa sifa ya kila Mkaazi .
CCM kimeitaja hatua ya kukosekana malalamiko toka Vyama vyote vya Siasa ni ishara na muendelezo wa kufanyika chaguzi huru na za haki Zanzibar.
Hayo yameelezwa Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi ,Uenezi na Mafunzo ,Khamisi Mbeto Khamis , aliyesema kila kitu katika zoezi hilo kimekwenda kwa murua.
Mbeto alisema wananchi walijitokeza kwa wingi ili kutumia haki yao ya msingi na ya kikatiba ili kujiandikisha na kuwa wapiga kura halali.
Alisema itakuwa vyema katika majimbo mengine hali ya utulivu ikaendea kama iliofanyika katika majimbo manne ya Wilaya ya Micheweni.
"CCM tumeridhishwa jinsi zoezi lilivyosimamiwa na maafisa wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar. Masheha wametimiza wajibu wao na kadhalika,".

0 Comments