DED KIBAHA MJI AFUNGA MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU KWA WATENDAJI NGAZI YA JIMBO



NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
 
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Kibaha mjini Dkt. Rogers Shemwelekwa amewataka watendaji ngazi ya Jimbo la Kibaha mjini lililopo Mkoa wa Pwani  kuhakikisha kwamba wanayatumia  kwa weledi  mkubwa mafunzo  ambayo wamepatiwa kuhusiana na suala zima la kusimamia kwa umakini zoezi zima la  uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa mwaka wa 2025.

Akizungumza  wakati wa kufunga  rasmi mafunzo  hayo ambayo yamefanyika kwa kipindi cha siku mbili  katika ukumbi wa Halmashauri ya mji Kibaha Mkurugenzi huyo  mewahimiza kuyatumia vizuri mafunzo  mbali mbali  ambayo wamepatiwa na kuyatumia  katika kipindi chote cha zoezi hilo la uboreshaji wa daftari  litakapoanza rasmi  kuanzia Februari 13 mwaka huu hadi Februari 19.

Dkt. Shemwelekwa anatambua mafunzo hayo ya siku mbili yameweza kuwaongezea ujuzi zaidi ikiwemo suala zima la ujazaji wa fomu mbali mbali ambazo zitatumika katika vituo,ikiwemo fomu  za kiapo kwa ajili ya kutunza siri na kujitoa uanachama katika chama cha siasa pamoja na zile za mkataba wa ajira kwa watendaji wa vituo.

"Nafahamu katika mafunzo haya meweza kujifunza kwa njia ya nadharia pamoja na vitendo jinsi ya namna ya kuandikisha wapiga kura kwa kutumia mfumo wa kujiandikisha wapiga kura ikiwa ni pamoja na kuchukua taarifa binafsi kwa lengo la kuweza kuchapisha kadi maalumu kwa ajili ya mpiga kura.

Aidha mkurugenzi huyo amesema kwamba lengo kubwa la semina hiyo ni kutoa mafunzo maalumu  ambayo yataweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika suala zima la utekelezaji wa zoezi la  uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura na kwamba elimu na ujuzi walioupata utaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kutekeelza kwa nadharia pamoja na vitendo.
Pia Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa watendaji hao ngazi ya Jimbo kuendelea kutumia muda wao wa ziada katika kusoma na kupitia maelekezo yote ambayo wamepatiwa ili kuonngeza uelewa zaidi kuhusu wajibu na majukumu yao katika zoezi zima la uandikishaji wa daftrai hilo la kudumu.

Katika hatua nyingine amewakumbusha  washirikia hao wapatao 308 kuzingatia umakini  katika kila eneo ikiwemo suala la utunzaji wa vifaa vya uandikishaji kwani vifaa hivyo vimenunuliwa na serikali kwa gharama kubwa hivyo vinapaswa kutunzwa kwani vinatarajiwa kutumika katika maeneo mengine ya uandikishaji nchini.

Nao baadhi ya washiriki katika mafunzo hayo wamepongeza Halmashauri hiyo kwa kuweza kuwapatia ujuzi na maharifa na kuahidi kwenda kuyatekeleza  kwa wananchi kwa  njia ya nadaria na vitendo kuhusiana na uboreshaji huo wa daftari ya kudumu la mpiga kura na kuongeza maelekezo yote  waliyopatiwa na Mkurugenzi watakwenda kuyafanyia kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu zote za nchi.

Kauli mbiu ya mwaka huu  wa 2025 katika zoezi hilo la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura  inasema kwamba kujiandikisha kuwa mpiga kura ni msingi wa uchaguzi bora.

Post a Comment

0 Comments