HALMASHAURI YA WILAYA YA BUKOBA YAPAMBANIA MAZINGIRA, ZAIDI YA MITI 280 YA MBAO YAPANDWA


Na Mwandishi Wetu 

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Halmashauri ya Bukoba Mkoani Kagera Mhe.Yassir Matsawily wakati akiongea na waandishi wa habari.

 Matsawily amesema kuwa wamepanda miti katika maeneo mbali mbali ya Halmashauri hiyo pamoja na kufanya shughuli nyingine ikiwa ni kuadhimisha miaka 48 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM.

Mhe.Yassir ameongeza kuwa wao kama jumuiya ya wazazi watahakikisha miti iyo inalindwa vyema ikiwa ni jitihada za kutunza mazingira.

Katika hatua nyingine kiongozi huyo amesema kuwa wao kama jumuiya ya wazazi Wilaya ya Bukoba wanampongeza sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa za kuendelea kuleta maendeleo katika Jimbo la Bukoba Vijijini hasa katika sekta ya Afya, Elimu, maji, miundombinu ya Barabara na miradi mingine kwenye Jimbo hilo na Mkoa kwa ujumla.

Aidha ameongeza kuwa kama jumuiya ya wazazi wilaya ya Bukoba wamejipanga kuhakikisha wanamtafutia kura za kutosha Rais Samia  pamoja na Makamu wake dokta. Emanuel Nchimbi katika uchaguzi mkuu unaotarijia kufanyika mapema mwaka huu.

 Yassir amesema kuwa kwa makubwa yanayofanywa chini ya uongozi Rais katika Nchi hii hawatatumia nguvu nyingi kwenye uchaguzi mkuu kwa kuwa kila kitu kinaonekana kwa macho.

Post a Comment

0 Comments