KIBAHA TC YAPITISHA MPANGO WA BAJETI YA BILIONI 57.5 MWAKA 2025/2026


NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
 
Halmashauri ya mji Kibaha  imepitisha mpango wa  bajeti wa jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 57.5  ya Halmashauri kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2025 hadi 2026 ambayo itakwenda kutumika katika matumizi ya kawaida pamoja na kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo sambamba na kutatua changamoto zinazowakabili a wananchi.

Akisoma taarifa katika kikao  cha baraza maalumu kwa ajili ya kupitisha mapendekezo ya  mpango huo Makamu  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibaha mji Karimu Mtambo amesema kwamba  kwa upande wa mapato ya ndani halmashauri imekisia kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 11.640 ikiwa ni ongezeko la asilimia 29 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka jana ambayo ilikuwa ni shilingi bilioni 8.

Makamu mwenyekiti huyo amesema kwamba Halmashauri hiyo imepanga kupelekea asilimia 60 ya fedha za mapato ya ndani kwenye miradi mbali mbali ya maendeleo na asilimia 40 kwenye matumizi ya kawaida na kwamba imepanga jkutekeleza kutekeleza miradi miradi ya kuongeza mapato ya ndani yenye thamani ya shilingi bilioni 1.49.

Aidha amesema kwamba katika bajeti hiyo fedha ndani itakwenda kutekeleza  miradi ikiwemo uboreshaji wa danpo la misugusugu, ununuzi wa gari la taka, ujenzi wa sehemu ya biashara,pamoja na kituo cha utoaji wa huduma katika kata za tumbi,maili moja, Kongowe,Mkuza pamoja na Tangini ikiwa pamoja na kujenga miundombinu ya biashara za machinga, sambamba na ujenzi kituo cha mafuta na karakana na ununuzi wa gari kwa ajili ya shughuli za ardhi.

Pia amebainisha kwamba kupitia bajeti hiyo kwa upande wa elimu msingi jumla ya vyumba vya madarasa 25, matundu ya vyoo 47,vitajengwa, ukarabati wa maadarasa saba, shule 1, pamja ana ujenzi wa shule mpya tatu na utengenezaji wa madawati 500 utafanyika.

Makamu huyo amesema kwa upande wa elimu sekondari ujenzi wa shule mpya 1,vyumba vya maadarasa 5,Bweni moja,na Bwalo 1 la chakula utafanyika pamoja na umaliziaji wa nyumba moja ya walimu,maabara, 4 na ofisi 2 za walimu sambamba na utengenezaji wa viti na meza vipatavyo 466.

Akizungumzia kuhusiana na upande wa afya amesema kwamba ujenzi wa kituo kimoja, cha afya na majengo matano  ya zahanati,yatafanyika,ukamilishaji wa wodi 1 ya kituo cha afya na vyumba tatu za watumishi utafanyika ikiwa pamoja na ukarabati wa kituo kimoja cha afya.

Kwa uapnde wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibaha mji Mussa Ndomba amesema kwamba katika bajeti hiyo wametenga kiasi cha shilingi milioni 60 kwa ajili ya kuboresha huduma za miundombinu ya maji katika baadhi ya kata kwa lengo la kuweza kuwaondolea changamoto ya  maji wananchi.

Pia amesema kwamba Halmashauri ya Kibaha mjini katika bajeti hiyo wametenga kiasi cha shilingi milioni 30 katika kata zote 14 kwa ajili ya kuweza kuboresha miundombinu ya barabara ili ziweze kupitika kwa urahisi katika kipindi chote.

Naye Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe. Silvestry Koka amepongeza mpango wa bajeti hiyo na kuimiza kuhakikisha kwamba fedha ambazo zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo zisimamiwe vizuri kwa ajili ya kuleta chachu ya maendeleo na kutatua kero za wananchi.

Koka ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kuweza kuweka mipango ya kuibua vyanzo vipya vyaa mapato amabvyo vitakwenda kusaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza mapato ya ndani na kuleta mabadiliko ya kimaendeleo kwa wananchi wa maeneo mbali mbali katika miradi ya elimu, afya, miundombinu ya barabara, pamoja na huduma ya maji.

Post a Comment

0 Comments