Na Mwandishi Maalum, Dodoma
CHAMA Cha Mapinduzi kimesema si Republican wala Democratic chenye uwezo wa kutaka Mamlaka kamili huko Marekani kama ambavyo ACT kinavyowadanganya wafuasi wake Zanzibar .
CCM kimesema sera ya ACT kutaka mamlaka kamili Zanzibar ni sawa kuandaa uasi unaorudisha nyuma maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa miaka sitini.
Matamshi hayo yametamkwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar , Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis, akijibu mapigo ya Mwenyekiti wa ACT Wazalendo ,Othman Masoud Othman.
Othman ndiye Makamo wa Kwanza wa Rais SMZ , alikuwa akihutubia mkutano wa hadhara huko Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja aliyesema mwaka 2025 ni wa kuipatia Zanzibar Mamlaka kamili.
Mbeto akijibu hoja hiyo, alimtaka Othman kuacha kuwadanganya wazanzibari kuwasimulia hadithi kongwe na kuwapa ahadi amabazo ACT Wazalendo hakiwezi kuzitekeleza.
Akitoa mfano ,Mbeto alisema Marekani yenye Muungano wa Mataifa 52 , hakuna hata nchi moja (jimbo)kati ya hizo ,yenye uwezo wa kutaka ipate mamlaka yake kamili ndani ya Taifa la Marekani
"Othman acha kudanganya na kutoa ahadi hewa . Wewe ni msomi wa sheria. Act hakina ubavu wa kuvunja Muungano wa Tanzania . Hata Florida, Ohio au California inayoweza kupata mamlaka kamili Marekani " Alisema Mbeto.
Aidha Mwenezi huyo aliwataka viongozi wa ACT kuacha propaganda hasi ambazo zimekuwa zikiwafanya wapuuzwe na wananchi toka mwaka 1995 kwa kunadi sera hiyo inayowakosesha ushindi kila uchaguzi Mkuu .
"Baada ya miaka sitini na moja ya Muungano ni wazimu mtu kufikiria kuvunja Muungano . Ujasiri ni kuzungumzia changamoto zinazoukabili Muungamo na kuzitatua si kupata mamkala kamili " Alieleza Mbeto
Alisema si taifa la Tanganyika wala Zanzibar ambalo kwa sasa linaweza kuibuka na kutaka mamlaka kamaili ndani ya Tanzania, kwa kufanya hivyo ni sawa na kuunda uasi au kufanya Mapinduzi
"Kila wakati watu wazima kudai mambo yasiowezekana ni kuonyesha wasivyo na maarifa.Acheni kupiga mayowe twendeni kwenye masanduku ya kura Oktoba mwaka huu mkakione cha mtemakuni " Alisisitiza Mbeto
Pia Mwenezi huyo alisema wakati kuna watanzania waliowekeza rasilimali ,mitaji na miradi yenye thamani kila yoande wa Muungano, hawatounga mkono sera hiyo isio na manufaa kwa maisha yao.
pia katibu mwenezi amewashukuru wananchi wa wilaya ya wete kwa kujitokeza kwa wingi kwenda kujiandikisha kwa amani na utulivu na kutimiza haki yao ya kikatiba na kisheria kwa kuzingatia kwamba ni haki ya kujiandikisha kwa mujibu wa sheria namba 4 ya mwaka 2018 ibara ya 15 ambayo ndio inasimamia suala la uandikishaji.
Wananchi wa wilaya ya wete yenye majimbo matano 5 ambao wote wameweza kupata fursa ya kujiandikisha kwa wingi na kutimiza matakwa ya sheria ya tume ya uchaguzi na kupata haki yao na fursa ya kujiandikisha ili wapate fursa ya kuja kuwachagua viongozi wao wakati ukifika wa uchaguzi mkuu October.

0 Comments