MWENYEKITI TLP LYIMO ASHAURI WANACHAMA WA VYAMA VYA SIASA KUJUA KATIBA ZAO, aeleza siri migogoro ndani ya vyama


Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) Richard Lyimo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Makao Makuu ya Chama Kinondoni mkoani Dar es Salaam. (Picha na Maktaba).

Na Mwandishi Wetu 

MWENYEKITI wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) Richard Lyimo ameshauri wanachama wa Vyama vya Saisa nchini kuhakikisha wanasoma na kuelelewa Katiba za vyama vyao ili kuepuka migogoro.

Lyimo alitoa ushauri huo mapema wiki  hii akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho Kinondoni mkoani Dar es Salaam.

Alisema migogoro mingi inayotokea ndani ya vyama imekuwa ikichangiwa na wanachama kitojua Katiba za vyama vyao hivyo kuanzisha madai ambayo ni kinyuma na kanuni na taratibu za Katiba zao.

Alitoa mfano wa kundi lililoibuka hivi karibuni na kulalamikia Mkutano Mkuu wa TLP uliofanyika Februari 2, Mwaka huu na kumchagua kuwa Mwenyekiti wa Chama kwamba ulikuwa na wajumbe feki, ambapo alisema kuwa kundi hilo halijui katiba ya Chama na kwamba walizoea zama za Chama kuendeshwa kimazoea pasipo kufuata Katiba.

Hata hivyo alieleza kuwa kundi hilo halijui madai halisi ya malalamiko yao kwani tayari walishafitwa uanachama tangu Oktoba 8 Mwaka Jana hivyo jambo la muhimu wanalotakiwa kufuata ni kutambua makosa yao na kurudi katika utaratibu wa kuomba uanachama upya.

Lyimo alisisitiza kuwa kundi hilo kuendelea kutumia nembo ya Chama hicho Wakati sio viongozi wala wanachama ni kinyume na taratibu za Chama hivyo aliwataka kuacha mara Moja.

"Watu wanaolalamika tulishawafukuza uanachama tangu Oktoba 8 Mwaka Jana, hivyo wanatakiwa kuangalia njia waliyotimia kulalamikia ni sahihi ama lah!! Mkutano Mkuu ndiyo ngazi ya mwisho Kwa uamuzi," alisema Lyimo na kusisitiza,

"Hivyo Mkutano Mkuu ulishahitimisha suala lao, Kwa sababu waliandika barua ya malalamiko na kutumia nembo ya Chama Wakati hawana mamlaka yoyote tumewasamehe, lakini wafuate taratibu na Sheria za Katiba ya Chama,".

Lyimo alibainisha kuwa miongoni mwa mikakati ya Chama ni kuhakikisha wanachapisha Katiba ya Chama kwa wingi na kuisambaza katika Ofisi zao Nchi mzima ili viongozi na wanachama waweze kuisoma na kuijua.

Kuhusu mikakati yake baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama, Lyimo alisema atahakikisha Chama kinakuwa na nguvu ya kuweza kuishauri Serikali lakini pia kuweza kushika Dola.

Kwamba atahakikisha Chama kinarudi na Kasi na kusambaa na kujulikana Nchi mzima Kwa kushirikiana na viongozi wenzake waliochaguliwa.

Kadhalika atahakikisha viongozi wake wa mikoani, Wilaya na ngazi za chini kabisa wanafanya kazi ya kukijenga Chama Kwa nguvu zote.

Post a Comment

0 Comments