NA VICTOR MASANGU
SHIRIKA lisilokuwa la kiserikali la Organization for Community Development (OCODE) katika kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kuwawezesha vijana walishindwa kuendelea na mfumo rasmi wa elimu limefanikiwa kuwafikia jumla ya vijana 830 ndani ya Manispaa ya Kinondoni na Halmashauri ya Bagamoyo kwa lengo la kuwawezesha vijana hao wanapata elimu bora jumuishi na ustawi wa kiuchumi.
Hayo yamebainishwa na Afisa Miradi wa shirika hilo la OCODE Elizabeth Francis wakati wa mkutano wa na baadhi ya wadau wanaoshirikiana nao katika kutekeleza miradi ili kuwa na uelewa wa pamoja na kuimarisha ushirikiano ambao ni viongozi wa Manispaa ya Kinondoni na wa Bagamoyo viongozi wa Kata(mbweni , Bunju Kunduchi na Kawe), walimu wakuu wa shule, wajumbe wa kamati za shule, viongozi wa serikali za mitaa, pamoja na wanafunzi.
Francis amebainisha kwamba kwa sasa vijana hao wanapatiwa mafunzo ya stadi za Maisha kwa lengo la kujitambua , kufanya maamuzi sahihi, kufikiri kwa kina , mahusiano sanifu baadaye kupelewa kusomea stadi za ufundi .
“Sambamba na kuwawezesha vijana hao OCODE inaendelea na uandikishaji wa wanafunzi wanaohitaji kurudi shuleni ambao wameshindwa kuendelea kwa sababu mbalimbali ili kuwawezesha kurudi shuleni na kutimiza ndoto zao” alisema Francis na kuongezea “ Tunaomba sana ushirikiano wenu katika kufanikisha kupata vijana hao ambao wanahitaji kurudi shuleni wafike ofisi zetu za kata kwa uandikishaji”, alisistiza.
Kadhalika Francis amesema kwamba kuna mafanikio makubwa ambayo yamepatikana kupitia shirika hilo la Ocode ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa walimu wanaotoa mafunzo kwa vijana hao, kuanzisha jumla ya vituo 21 na kugawa vifaa vya ufundishaji katika vituo hivyo na kuanzishwa kwa vikundi vya kuweka na kukopa kwa kinababa na kinamama.
Kwa upande wake Afisa Mradi miradi ya Elimu, Tunu Sanga, amebainisha kwamba kwa upande wa Kuboresha ujifuzaji wa wanafunzi mashuleni shirika limetoa Mafunzo ya elimu jumuishi kwa walimu, kugawa viti, meza, pamoja na shelfu kwa darasa la awali katika shule ya Mbweni
Aidha, aliongeza kuwa shirika linapanga kufanya ukarabati wa madarasa katika shule za msingi za Kawe, Mbweni, na Mtongani, na pia kugawa viti, meza, na shelfu za kuhifadhia vitabu katika shule hizo na kwamba hivi karibuni shirika litatoa mafunzo kwa kamati za shule na kujengea uwezo kamati za UWAWA.
Afisa Maendeleo ya Jamii ambaye pia ni Focal Person wa Mradi kutoka Manispaa Furaha Libangu amesema kuwa vikundi vyote vilivyoanzishwa na shirika la OCODE yeye atavisimamia na kuhakikisha kuwa vinasajiriwa na fedha zao ziwekwe bank kwa lengo la kuwa salama Zaidi.
Naye Afisa Kilimo wa Manispaa ya Kinondoni amelipongeza kwa dhati shirika hilo la OCODE kwa jitihada zake za kuisaidia serikali na kuahidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika kusaidia miradi hiyo. Alisisitiza kuwa Kinondoni kuna chuo cha uvuvi, na aliomba ushirikiano ili vijana wanaohitaji kujifunza uvuvi waweze kujiunga na chuo hicho kwa bei nafuu.
0 Comments